29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

MAHAKAMA YAFUTA MAUZO HISA ZA TIGO

                                                                |Kulwa Mzee, Dar es SalaamMahakama ya Rufaa ya Tanzania, imefuta mauzo ya hisa za Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo kwa sababu yalifanyika kwa udanganyifu.

Uamuzi wa mahakama hiyo umetolewa leo Alhamisi Julai 26, na Msajili wa mahakama hiyo, John Kahyoza kwa niaba ya jopo la majaji lililoongozwa na Jaji Stella Mugasha, Jaji Rehema Mkuya na Jaji Jacob Mwambegele.

Mdai katika kesi hiyo ni Milicom (Tanzania) NV dhidi ya James Bell, Golden Globe International Services limited, Quality Group, Mic UFA Limited, Milicom International na Michezo Tanzania Limited.

Katika uamuzi wake, Kahyoza amesema malalamiko ya mlalamikaji yameonekana kuwa ya msingi, na kwamba mauzo ya hisa 34,479 zenye thamani ya Sh bilioni 13 yalifanyika kwa udanganyifu.

Hivyo, jopo hilo liliamua kuyafuta mauzo hayo kwani hayakuwa sahihi na kuamuru aliyenunua hisa hizo arejeshewe fedha zake.

Soma zaidi… https://mtanzania.co.tz/tuhuma-nzito-yagubika-kesi-hisa-za-tigo/

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,335FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles