27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yaamuru upelezi kesi ya maofisa LHRC ukamilike haraka

NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru upelelezi katika kesi inayomkabili Ofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHCR), Tito Magoti na mwenzake ukamilike haraka.

Uamuzi huo wa mahakama ulitolewa jana baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha hoja kwamba watajitahidi upelelezi ukamilike.

Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mtega, alidai shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado unaendelea.

“Tulifanya mawasiliano na wapelelezi kama mahakama ilivyoelekeza kukamilisha upelelezi haraka, wapelelezi wameahidi kukamilisha upelelezi sababu maeneo yanayopelelezwa ni mengi lakini watajitahidi wakamilishe,”alidai Mwankyo.

Wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya akijibu alidai wamesikia jitihada za upande wa Jamhuri hivyo wanaomba wakamilishe upelelezi kwani  unachukua muda mrefu na makosa yenyewe yanaonekana kama yalishapelelezwa kabla ya kushtakiwa.

“Tunaomba wamalize upelelezi mapema ili kesi isikilizwe na washtakiwa wapate nafasi ya kusikilizwa kisha mahakama itoe uamuzi,”alidai Mtobesya.

Wankyo aliahidi kwamba watayafanyia kazi maombi yao.

Hakimu aliamuru upelelezi umalizike haraka ili kesi hiyo iendelee katika hatua nyingine. Kesi iliahirishwa hadi  Aprili 29 mwaka huu kwa kutajwa.

Mbali na Magoti, mshtakiwa mwingine ni Mtaalamu wa Tehama, Theodory Giyani (36).

Katika kesi hiyo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kumiliki programu ya kompyuta iliyotengenezwa mahususi kufanya kosa la jinai na kuwawezesha kujipatia  Sh 17,354,535, kumiliki programu ya kompyuta iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya kutenda makosa ya jinai na kujipatia jumla ya Sh 17,353,535 huku wakijua mapato hayo yametokana na mazalia ya kosa la kushiriki genge la uhalifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles