24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA YAAMURU KIGOGO IPTL KUTIBIWA MUHIMBILI

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru Kigogo wa IPTL, Habinder Sethi apelelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili akatibiwe hali yake kiafya imeharibika.

Uamuzi huo umetolewa leo asubuhi Jumatano Machi 28, baada ya mshtakiwa kueleza kwamba hali yake imeharibika sana hivyo anaomba akatibiwe.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi amesema mshtakiwa anaumwa na anaonekana hata kwa macho hivyo hawezi kuendelea na shauri wakati mtu akiwa mgonjwa hivyo ambapo aliamuru akatibiwe Muhimbili.

Pamoja na Habinder na James Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka ya mbalimbali ya uhujumu uchumi ikiwemo kutakatisha fedha.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles