24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yaamuru dhamana kwa kigogo ZSTC

Khamis Sharif -Zanzibar

MAHAKAMA Kuu Zanzibar imeamuru kupewa dhamana kwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC), Seif Suleiman Kassim (58), ambaye anakabiliwa na kesi ya ubakaji wa mwanafunzi wa miaka 13 Aprili mwaka jana.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mkusa Isack Sepetu, baada mahakama hiyo kujiridhisha na maombi ya dhamana ya mtuhumiwa huyo ambayo yaliwasilishwa Januari mwaka huu.

Miongoni mwa sababu zilizomtoa nje mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa mahabusu kwa muda miezi miwili, ni pamoja na wadhifa alionao kwenye eneo lake la kazi.

Jaji Sepetu alisema mahakama imejiridhisha na hoja za mtuhumiwa huyo na ikiwamo kama akiendelea kukaa mahabusu kungeathiri shughuli nyingine za kitaifa, hasa kutokana na msimu huu wa uvunaji wa zao la karafuu ambalo ndilo kinara wa uchumi wa Zanzibar.

Kutokana na sababu hizo ambazo Jaji Mkusa alikubaliana nazo, ndipo mtuhumiwa huyo Januari 7, mwaka huu alipewa dhamana baada ya kutimiza masharti.

“Baada ya kupitia maombi yako ya dhamana na sababu ambazo umeziainisha, mahakama hii inakupa dhamana yenye masharti ya Sh 500,000 za maandishi na wadhamini wawili wenye kima kama hicho kila mmoja,” alisema Jaji Mkusa.

Sharti jingine ni mtuhumiwa huyo kuhakikisha hasafiri nje ya Kisiwa cha Pemba bila ya kibali cha jaji husika.

Awali ilidaiwa kuwa tarehe isiyofahamika Aprili mwaka jana, saa 6 mchana, eneo la Bandarini mkoani Pemba, mtuhumiwa huyo alimtorosha mtoto wa miaka 13 ambaye ni mwanafunzi bila ridhaa ya wazazi wake.

Inadaiwa mtoto huyo alitoroshwa alipokuwa anakwenda shule na kisha kumwingiza kwenye ofisi anayofanya kazi ya ZSTC iliyopo bandarini Mkoani.

Kutorosha ni kosa kinyume na kifungu cha 113 (1) (a) cha Sheria ya adhabu namba 6 ya mwaka 2018, Sheria ya Zanzibar.

Kosa la pili linalomkabili mtuhumiwa huyu, ni ubakaji wa mtoto ambae jina limehifadhiwa, ambapo kufanya hivyo ni kosa na pia kinyume na kifungu cha 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya adhabu No 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles