27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama ya mafisadi yaanza kasi rasmi

othmanchandeNA KULWA MZEE
-DAR ES SALAAM

JAJI Mkuu, Mohammed Chande amesema Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi imeshaanza kazi.

Alisema sheria na kanuni zake zimekwisha kuchapwa katika Gazeti la Serikali namba 267 Septemba 9 mwaka huu.
Jaji Chande alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania na mradi wa maboresho ya huduma za mahakama .

“Kanuni kwa ajili ya kuendesha Mahakama ya Mafisadi zinaelekeza kesi inafunguliwa vipi, kesi inapangiwa jaji ndani ya siku moja, inasomwa maelezo ya awali ndani ya siku 30 .

“Kanuni zinaelekeza jinsi ya kumlinda shahidi, shauri litasikilizwa na kumalizika kwa miezi tisa na endapo kutakuwa na sababu kuna ongezeko la miezi sita, kama itatokea sababu nyingine mahakama itaangalia muda.
“Uzuri wa mahakama hii anayechelewesha kesi atajulikana, shauri likiahirishwa bila sababu ya msingi anayesababisha anaweza kuamuriwa na jaji kulipa gharama ya Sh 150,000.

“Taratibu zimeshawekwa majaji wameshamaliza mafunzo na wameteuliwa 14, uwazi ni muhimu katika kutoa haki kwa mshtakiwa ili apate fursa ya kujitetea. Mahakama haitakuwa ya kuahirisha kesi bila ya sababu za msingi,”alisema.

Jaji Chande alisema mahakama inatarajia kuzindua mpango mkakati wa miaka mitano, 2015-2020 na mradi wa maboresho ya huduma za mahakama ambao shirikishi kati ya Serikali , mahakama na Benki ya dunia.

“Mpango mkakati utagharimu Sh bilioni 238 na mradi wa maboresho utagharimu Sh bilioni 140, vyote vitazinduliwa Jumatano katika Mahakama ya kisasa ya Wilaya ya Kibaha ambako mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais Dk. John Magufuli,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles