24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama ya mafisadi kupelekwa mikoani

Othman Chande

NA JANETH MUSHI, ARUSHA

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha inatarajiwa kuwa moja ya masijala ndogo ya mahakama ya mafisadi inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao na majaji, mahakimu na watumishi wa mahakama za mikoa ya Arusha na Manyara.

Alisema masijala kuu ya mahakama hiyo ambayo ukarabati wa jengo lake lililopo Sinza jijini Dar es Salaam umeshaanza na mahakama za kanda nyingine za Mahakama Kuu zitakazokuwa masijala ndogo ni pamoja na Tanga, Mbeya na Mwanza.

“Masijala kuu itakuwa Dar es Salaam ila kutakuwepo na masijala ndogo katika Kanda za Mahakama Kuu ambapo kesi zitaweza kufunguliwa katika masijala hizo.

“Rasimu ya kwanza ya uanzishwaji wa mahakama hiyo inapitiwa na iko katika hatua za mwisho, ikikamilika itatangazwa katika gazeti la Serikali na itatoa mwongozo wa taratibu na kanuni inayoeleza utafungua wapi kesi na inaeleza jinsi kesi itakavyoandikwa na taratibu nyingine zote,” alisema Chande.

Kuhusu utendaji kazi wa mahakama katika kipindi cha Januari hadi Juni, mwaka huu, alisema katika kipindi hicho, mahakama 54 za mwanzo za mikoa ya Arusha na Manyara zimefanya kazi ya kuridhisha na kesi 6,485 zimeshatolewa uamuzi huku kesi 1,198 zinazoendelea kusikilizwa zikiwa chini ya miezi sita.

Jaji Chande alisema walikubaliana mahakama za mwanzo kusikiliza kesi katika kipindi cha miezi sita na hadi sasa katika mikoa hiyo kesi 19 ndizo hazijamalizwa kusikilizwa huku zikiwa na muda wa zaidi ya miezi sita tangu zipelekwe mahakamani hapo.

“Tulikubaliana hakimu wa mahakama za mwanzo wasikilize kesi 260 kwa

mwaka, katika mikoa hii kuna mahakimu  55 na kila mmoja ameamua kesi 117, nimewaagiza hakimu asiye na kesi kituoni kwake akasaidie wenzake kwenye vituo vingine,” alisema Jaji Chande.

Kuhusu miundombinu mibovu ya mahakama hapa nchini, alisema hivi sasa wana mkakati wa kitaifa wa kuboresha majengo ya mahakama na kwa Arusha na Manyara, mahakama 18 za mwanzo zimefungwa kutokana na miundombinu yake kuchakaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles