24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA, TLS WAKUBALIANA KUSHIRIKIANA

                                                                |Kulwa Mzee, Dar es Salaam


Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume na viongozi wengine wamekutana na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma na kuelezwa mpango mkakati ambao ndiyo dira ya mahakama.

Uongozi huo wa TLS umekutana na Jaji Mkuu na wadau wengine wa mahakama leo Jumanne Julai 24, ambapo Msajili Mkuu wa Mahakama, Catherine Revocati pamoja na mambo mengine amesema hiyo ni fursa ya kuanza kushirikiana.

“Mpango mkakati ndiyo dira ya mahakama, tunaomba ushirikiano katika eneo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama),  lazima tubadilike, twende dunia inavyokwenda, tuachane na matumizi ya karatasi.

“Mawakili ni wadau wetu muhimu, bila wao sisi hatuwezi kufanya kazi, na wao bila sisi hawawezi kufanya kazi, tulianza nao, wameanza kujiandikisha katika mfumo mpya, tunaomba muendelee kutupigia debe waendelee kujiandikisha,” amesema Revocati.

Kwa upande wake Rais wa TLS, Fatma amesema mahakama haiwezi kuboresha mazingira ya utoaji haki katika maamuzi kama hawatazungumza na TLS.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles