25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama Kuu yazuia uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki

MWANDISHI WETU-DODOMA

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma, imetoa zuio la kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Arumeru Mashariki hadi uamuzi wa kesi au maombi madogo ya kufungua kesi ya msingi ya kuomba kutengua uamuzi wa Spika Job Ndugai wa kumfutia ubunge Joshua Nassari itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Akizungumza jana mjini Dodoma Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, Dayness Lyimo, alisema kesi hiyo namba 22 ya mwaka 2019 inasikilizwa chini ya Jaji Latifa Mansoor.

Alisema wajibu maombi katika kesi hiyo ni Spika wa Bunge  na mwanasheria mkuu wa Serikali ambao wamepewa siku saba kupeleka kiapo kinzani cha maombi hayo.

“Jaji pia ameagiza kusifanyike uchaguzi wowote (jimboni) hadi hapo maombi hayo yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi,” alisema.

Wakati hayo yakiendelea Nassari alikuwapo mahakamani hapo, huku akiwakilishwa na mawakili watatu ambao ni Hekima Mwasipe, Jonathan Mndeme na Fred Kalonga.

Upande wa walalamikiwa unawakilishwa na wakili wa Serikali Masunga Kawahanda.

Kesi hiyo itakwenda tena mahakamani Machi 27 kwa ajili ya kusikilizwa.

Akizungumzia uamuzi huo, Nassari alisema baada ya kusikiliwa kwa hoja za pande zote mbili, Mahakama Kuu imetoa siku saba, ambapo aliishukuru kwa uamuzi wake.

Mapema wiki hii katika mkutano wake na waandishi wa habari, Nassari alisema anakusudia kwenda mahakamani kudai haki ya uwakilishi wa wananchi wa Arumeru baada ya Spika Ndugai kutangaza kwamba hana sifa za kuendelea kuwa mbunge.

Vile vile alisema Spika bado anayo nafasi ya kurejea uamuzi wake ili wananchi wa Arumeru Mashariki waendelee kuwa na mwakilishi bungeni.

Katika utetezi wake Nassari alisema mara ya mwisho alihudhuria mkutano wa Bunge wa Septemba lakini hakuhudhuria mkutano wa Novemba na Januari kwa sababu alikuwa anamuuguza mke wake nje ya nchi.

“Nasikitika kwa uamuzi alioufanya, nawapa pole wananchi wangu wa Arumeru, haki yao tutaitafuta kwenye vyombo vya sheria,”alisema Nassari.

Akizungumza huku akitokwa na machozi, Nassari alisema alikuwa akimwuguza mke wake kutokana na matatizo aliyokuwanayo na kwamba alijaliwa kupata mtoto wa kike Januari 27 mwaka huu, siku moja kabla ya kuanza   mkutano wa Bunge la Januari.

Mei 14  Spika wa Bunge, Job Ndugai alimwandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage kumtaarifu Jimbo la Arumeru Mashariki liko wazi kutokana mbunge wake (Nassari) kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles