24.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Mahakama Kuu yatupa pingamizi uuzwaji hoteli Tai Five

Na BENJAMIN MASESE – MWANZAMAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza, imetupilia mbali mapingamizi mawili yaliyowekwa na wakili wa upande wa mlalamikiwa namba mbili, mfanyabiashara wa mabasi ya Batco, Baya Malagi, kwenye kesi ya mauziano ya Hoteli ya Tai Five ya   Mwanza.

Kesi hiyo ya madai ya ardhi namba 46 ya mwaka  2017 ilifunguliwa na aliyekuwa mmiliki wa hoteli hiyo iliopo Nyamanoro jijini hapa, Christopher Tarimo, mwaka 2017 katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Issa Maige alitoa hukumu hiyo jana katika kesi ya msingi.

Alisema   mapingamizi ya  sheria yaliyowekwa na wakili upande wa mlalamikiwa namba mbili, mfanyabiashara Kusaga Malagi   hayana msingi.

Mapingamizi hayo mawili yalikuwa ni kufanana kwa shauri lililokuwapo mahakamani hapo mwaka 2011 na pingamizi jingine lililowekwa, kuwa ni usumbufu kwa mahakama kusikiliza kesi kwa mara nyingine.

Upande wa mujibu maombi namba moja ambayo ni  Benki ya CRDB uliwakilishwa na Wakili Galati Silwane,  huku upande wa mlalamikiwa namba mbili ukiwakilishwa na Wakili Emmanuel Anthony.

Upande wa mlalamikaji Christopher Tarimo uliwakilishwa na mawakili Julius Mushumbusi na Mwita Emmanuel kutoka Kampuni ya Wanasheria ya Kailu Law Chembers.

Baada ya kusikilizwa  pande zote mbili kuhusu hoja hizo, Jaji Maige alisema  mahakama imeona kulikuwa na utata mkubwa katika mauziano ya Hoteli ya Tai Five yaliyofanyika kati ya mlalamikiwa namba moja na mbili.

Jaji alisema   mauziano hayo pia yalighubikwa na  mambo ya sintofahamu  na  kwamba mauziano hayo yalifanyika bila kukazia hukumu ya kesi namba 4 ya 2011.

Pia alisema mauziano ya wajibu maombi yanaonekana kama yalifanyika baina ya waleta maombi  ambao ni Tai Five Ltd na Christopher Tarimo na mjibu maombi namba moja  ambayo  ni The Mogeji Instruments.

Waandishi walipomtaka wakili wa upande mlalamikaji, Mwita Emmanuel  kuzungumzia uamuzi huo alidai suala hilo wanaiachia mahakama yenye mamlaka ya kutenda haki.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,400FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles