30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Mahakama Kuu kusikiliza rufaa ya Mbowe, Matiko kupinga kufutiwa dhamana leo

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imefurika wafuasi wa Chadema waliofika kusikiliza rufaa ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wanaosota gerezani baada ya kufutiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wiki iliyopita.

Rufaa hiyo inasikilizwa leo Jumatano Novemba 28, asubuhi hii na watuhumiwa wako mahabusu ya mahakama wakisubiri muda wa kupanda kizimbani.

Jaji Sam Rumanyika ndiye atasikiliza rufaa hiyo iliyokatwa na viongozi hao kupinga umuzi wa kufutiwa dhamana kupitia jopo la mawakili wao akiwamo Peter Kibatala.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya jana washtakiwa hao kupelekewa hati za kuitwa leo kwenye shauri lao.

Mbowe na Matiko walifutiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya kuonekana wanaoidharau mahakama kwa kutohudhuria katika kesi yao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,951FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles