30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA KUU KUJENGA KITUO MAALUMU

 

 

NA MAGRETH KINABO-DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Tanzania kupitia mpango  mkakati  wake wa miaka mitano wa 2015- 2020, inatarajia kujenga kituo maalumu ikiwa ni hatua ya kupanua wigo  wa huduma  kwa watu wenye mahitaji maalumu.

Kuanzishwa kwa kituo ni hatua ya kuwapunguzia wananchi gharama za fedha  wanazozitumia, muda wanaoutumia  na utoaji wa haki kwa wakati.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Mkutano wa Mashauriano kuhusu  uanzishaji Kituo Maalumu cha kushughulikia masuala ya mirathi  ambaye ni Msajili ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Ilvin  Mugeta.

“Tuna  mpango wa kuanzisha  kituo hicho cha  huduma  za  mahakama   kuhusiana  na masuala  ya mirathi, ambacho  kitakuwa na wadau  mbalimbali wa Mahakama  ya Tanzania   kuhakikisha  huduma za mirathi  zinatolewa kwa wakati  bila kupoteza muda  na gharama,” alisema.

Alisema kituo hicho pia kitasaidia  kupunguza mlundikano  wa  kesi  zilizokaa muda mrefu mahakamani, ikiwa ni moja ya mkakati wa mahakama wa kupitia mpango huo.

“Katika  mpango huo mahakama  inatarajia kujenga  kituo   cha pamoja kitakachoshughulikia masuala ya mirathi.

“Hivyo huduma  hizo zitakuwa zinapatikana kwenye jengo moja   kuwaondolea usumbufu   watu wanaohitaji huduma za mahakama,” alisema  Mugeta.

Alisema kituo hicho  kitakuwa  na huduma  za  Mahakama  ya Mwanzo,  Mahakama ya Wilaya na Mahakama Kuu   na kusaidia watu wanaohitaji huduma hiyo kupatiwa haki zao kwa wakati.

Kituo  hicho cha pamoja   kinatarajiwa kuanza kufanya kazi Dar es Salaam mwaka 2019 katika Wilaya ya Temeke karibu  na Kituo cha  Polisi Chang’ombe ,  eneo ilipo Mahakama  ya Mwanzo  Temeke.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles