31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

MAHAKAMA 20 KUJENGWA DAR

Na MAULI MUYENJWA-DAR ES SALAAM


paul-makondaMAHAKAMA za mwanzo 20 zinatarajiwa kujengwa katika maeneo mbalimbali Dar es Salaam, ili kurahisisha upatikanaji wa haki.

Ujenzi huo ambao unasubiri ramani kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, utasimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alisema kutokana na changamoto ya upatikanaji wa haki katika jiji hilo, wameamua kujenga mahakama hizo ili wananchi wengi waweze kupata haki kwa wakati.

“Tunasubiri ramani tutakayopewa na Mahakama Kuu kisha mwakani tutaanza ujenzi huo, kwa sasa bado tunaendelea na ujenzi wa vituo vya polisi, lakini tukiwa na mahakama itasaidia wananchi wengi wenye shida.

“Yeyote anaweza kuchangia ujenzi huo, lakini si kwamba ndiyo atakuwa huru kufanya makosa, akifanya kosa atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria,” alisema Makonda.

Naye Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema pamoja na ujenzi wa mahakama hizo, bado kuna tatizo kubwa la nidhamu na maadili ya watendaji wa mahakama.

“Tumeunda kamati za maadili za mahakimu wa mahakama za mwanzo, ambazo wakuu wa wilaya ni wenyeviti, lakini wananchi ambao wanakutana na mahakimu wenye matatizo, ni haki yao kuwashtaki kwa katibu tawala ili wachukuliwe hatua, na kufanya hivyo hatuingilii uhuru wa mahakama,” alisema Dk. Mwakyembe.

Alisema kuwa uchache wa kesi katika mahakama ya mafisadi ndiyo mafanikio makubwa kwa hatua ya kuanzisha mahakama hiyo.

“Uwepo wa mahakama hiyo unasaidia watu kuogopa kufanya ufisadi wa fedha nyingi, lakini hata hivyo Serikali ikiona kama wizi wa kiasi cha Sh milioni 400 au 500 unakithiri, inaweza kushusha kiwango cha fedha kwa mahakama hiyo ili na wao washughulikiwe na mahakama hiyo,” alisema Dk. Mwakyembe.

Hata hivyo, alisema hatua ya Makonda kuanzisha utaratibu wa kuwatumia wanasheria vijana ambao watakuwa wanatoa elimu ya kisheria kwa wananchi mbalimbali ambao hawana uelewa juu ya sheria, ili iwasaidie katika kesi zao waweze kupata haki ni mzuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles