Maguire: Man United ‘Top-Four’ inatuhusu

0
864
Harry Maguire

MANCHESTER, ENGLAND

BAADA ya timu ya Manchester United kufanikiwa kuondoka na pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City, beki wa timu hiyo Harry Maguire, amedai wana nafasi kubwa ya kuingia katika nafasi nne za juu.


Mchezo huo ulipigwa mwishoni mwa wiki iliopita huku Manchester City wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani Etihad, lakini walikubali kuwaachia pointi tatu wapinzani hao kwa kufungwa kichapo cha mabao 2-1.


Ushindi huo umemuweka sehemu salama kocha wa timu hiyo Ole Gunnar Solskjaer ambaye alikuwa hatarini kufukuzwa kutokana na mwenendo mbaya wa timu. Uongozi wa United ulimpa kocha huyo michezo miwili ikiwa pamoja na ule dhidi ya Tottenham mapema wiki iliopita, lakini United ikafanikiwa kushinda mabao 2-1.


Wachezaji wa Man United, walisema wapo tayari kujitoa kwa kila namna ili kuhakikisha wanampigania kocha wao, hivyo amefanikiwa kushinda michezo yote miwili na kujiweka salama.


Kutokana na ushindi huo wa michezo miwili, beki wa kati wa timu hiyo Maguire, amedai watahakikisha wanapambana ili kumaliza nafasi moja kati ya nne za juu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here