24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

MAGUFULI,WASTAAFU WATETA MAMBO MAZITO

Na MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM


*Sumaye aeleza safari ya upinzani ilivyopotoshwa

*Mwinyi avutiwa utendaji kwa wafanyakazi wa umma

*Lowassa ataka viongozi wapime athari za kauli zao

RAIS Dk. John Magufuli amekutana na viongozi wastaafu kujadiliana mambo mbalimbali ya mustakabali wa taifa.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa kudumisha amani kwa kuhakikisha haki inapatikana.

Rais Magufuli aliwakaribisha viongozi hao Ikulu, Dar es Salaam jana, ili ajadiliane nao kuhusu hali ya nchi na wamweleze yale waliyoona ametekeleza na kumshauri pale alipoteleza.

“Kwangu ni heshima kubwa kukutana nanyi leo, mmenipa heshima kubwa kuitika wito wangu na kuja hapa wengi wenu mmeacha kazi zenu.

“Nina bahati kuwa kiongozi wakati viongozi wengi wakiwa bado hai, ni sehemu chache duniani kuwa kiongozi halafu wale waliokutangulia wakiwa bado wapo, nashukuru sana,” alisema.

Pia aliwaeleza viongozi hao juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali hivi sasa, ikiwamo kuongeza ukusanyaji wa mapato ambao umeongezeka kutoka Sh bilioni 800 hadi Sh trilioni 1.3.

“Ninawahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea vizuri na kwamba itaendelea kutatua changamoto ambazo bado zipo kwa juhudi kubwa ili Tanzania iwe nchi nzuri kwa Watanzania wote,” alisema.

Katika mkutano huo wa kwanza Rais Magufuli kukutana na viongozi hao wakuu wastaafu, alipokea ushauri na maoni yao juu ya uendeshaji wa Serikali na mustakabali wa taifa.

Viongozi hao walimshukuru Rais Magufuli kwa kuwaita kwa lengo la kusikiliza ushauri na maoni yao, na wamempongeza kwa kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi kifupi cha miaka miwili na nusu tangu ilipoingia madarakani.

kwa habari kamili jipatie gazeti lako la MTANZANIA hapo juu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles