29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 30, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli: Wizara ya Mambo ya Ndani inanitesa

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais John Magufuli amekiri kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni miongozi mwa changamoto zinazomtesa.

Rais amesema hayo leo Alhamisi Januari 23, wakati akizindua nyumba za askari magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.

“Tuna changamoto nyingi kama, kuna wizara inanitesa ni Wizara ya Mambo ya Ndani, nataka muelewe hivyo Watanzania, inatesa sana.

“Zungu (Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan) atakumbuka tangu tumeingia madarakani katika kipindi cha miaka minne kuna tume nyingi zimeundwa kwa ajili ya kuchunguza tu Wizara ya Mambo ya Ndani kwenye miradi ya ovyo yaliyokuwa yakifanyika,” amesema Rais Magufuli.

Akielezea moja ya mkataba uliomkera Rais Magufuli amesema ni ule ulioingiwa na wizara hiyo na kampuni moja kutoka Romani wenye thamani ya Euro milioni 408.

“Hivi karibuni kulikuwa na mkataba mmoja wa ajabu unatengenezwa na wizara ya mambo ya ndani una thamani ya Euro milioni 408, sawa na trilioni na moja na kitu umetayarishwa na kusainiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto, haujapangwa kwenye bajeti wala haujapitishwa na bunge.

“Wakati wa vikao na kamupnui moja kutoka Romania wahusika wote wa Tanzania walipokuwa wanakwenda kwenye majadiliano pale wanalipwa kwanza posho ya kikao Dola 800 bado ya kulipiwa tiketi za ndege,” amesema.

Amesema mradi wa ovyo umesainiwa kule lakini ya ndani imeelezwa ukitaka kuuvunja yale ambayo yameanza kutekelezwa lazima yaendelee kutekelezwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles