29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli: Viongozi epukeni kuongoza kwa mazoea

Anna Potinus

Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa amewataka viongozi wa chama hicho kuepuka uongozi wa mazoea na badala yake wapige vita rushwa, uzembe na mambo mengine yanayowachelewesha kufikia malengo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Desemba 12, alipokuwa akifungua semina ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho Taifa (NEC) iliyofanyika Jijini Mwanza.

“Tuepuke uongozi wa mazoea na kusema ukweli vyama vingi vilivyojisahau na kuongoza serikali kwa mazoea vilifikia hatua ya kupoteza imani ya wananchi na uhalali wa kisiasa, hiki ndicho kilichotokea kwa baadhi ya vyama vingi vilivyopigania uhuru barani Afrika hivyo niwaombe ndugu zangu tusifikie huko.

“Nia yetu kubwa ni kujenga taifa linalojitegemea kiuchumi, ni lazima tupige vita rushwa, uzembe na mambo mengine yatakayotuchelewesha kufikia malengo yetu, ninachokiona mimi bado kuna uzembe, kushindwa kuchukua maamuzi na kupenda fedha za dezo na haya yote yanatokana na mazoea ya utegemezi.

“Kwa miaka mingi CCM ilikuwa shamba la bibi kila mtu alikuwa anatafuna mali na hivyo tukaanza kazi ya kurejesha mali za chama ikiwemo vyombo vya habari kama Channel ten ambayo pamoja na kwamba ilikuwa ni mali ya chama lakini ilikuwa chini ya usimamizi wa watu wengine, tukarejesha majengo, viwanja, vitalu vya madini, vituo vya mafuta na pia tukanza kupitia mikataba mbalimbali ya biashara na uwekezaji ndani ya chama,” amesema Rais Magufuli.

Aidha ameongeza kuwa chama hicho kimeendelea kunufaika kwani kupitia wanachama mbalimbali kutoka vyama vya upinzani wakiwemo wabunge na madiwani waliowapokea katika miaka minne iliyopita kupokea wamepelekea ruzuku ya chama kuongezeka kutoka Sh bilioni 12.4 kwa mwaka 2015/16 hadi bilioni 13.5 kwa mwaka hivi sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles