Magufuli: Uongozi ni utume

0
791
Rais Dk. John Magufuli akimuapisha, Mathias Kabunduguru, kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Ikulu Dar es Salaam jana.

ANDREW MSECHU-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amewataka viongozi aliowateua kwenda kufanya kazi na kutatua matatizo ya wananchi, kwa kuwa uongozi ni kazi ya kitume.

Akizungumza wakati wa kuwaapisha viongozi aliowateua wiki iliyopita Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema kazi za watu ni utume na wakawatumikie Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake.

“Kazi hizi zina challenge (changamoto) kubwa lakini kikubwa ni kumtanguliza Mungu na kufanya kazi zenu bila kumuonea mtu, kwa kadiri mioyo na Mungu wenu atakavyowatuma kuwatumikia.

“Kwa hiyo saa nyingine katika kazi za uongozi inahitaji uvumilivu na kumtanguliza mbele mwenyezi Mungu. Wakati mwingine unaweza kusemwa tu vibaya ila kasimamieni haki. Kazi hizi ni lazima wakawatumikie wananchi hasa wanyonge,” alisema.

Alielezea ziara yake mkoano Mtwara ambako aliongozana na Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rishwa (Takukuru), Brigedia Jenerali Mbungo ambapo walikuta malalamiko ya baadhi ya watu ambao wamedhulumiwa malipo ya korosho kuanzia 2016 hadi 2017.

Alisema walibaini kuwa katika dhuluma hiyo ilihusisha vyama vya ushirika 10 lakini Brigedia Jenerali, akukuta ni vyama 32 vya ushirika vilivyokuwa vinawadhulumu.

Rasi Magufuli alisema awali walijua kuwa wakulima hao wamedhulumiwa Sh milioni 80 lakini baada ya kufuatilia walikuta wananchi wamedhulimiwa Sh bilioni 1.2 na wameweza kushika viongozi 92 na hadi juzi, Sh milioni 255 zilikuwa zimesharudishwa na nyingine zitaendelea kurudishwa.

“Kwa hiyo unaweza kuona mtu amelima korosha yake ameeuza korosho yake tangu 2016 hadi 2017 anadai hadi amaeshakata tamaa, zaidi ya Sh bilioni 1.2 iko kwenye vyama vya ushirika vya Amcos, kwahiyo unaweza kuona dhuluma inavyotendeka kwa wananchi hasa wanyonge.

“Tuna jukumu la kutetea hawa wanyonge na kufuta machozi yao na kwamba hata hizo milioni 255 zilizopatikana ni mwanzo mzuri na mimehakikishiwa watazitema zote,” alisema.

Walioapishwa jana ni Mathias Kabunduguru ambaye sasa ndiye Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, akichukua nafasi ya Hussein Katanga aliyeteuliwa kuwa balozi.

Wengine ni Godfrey Mweli anayekuwa Naibu Katibu Mkuu Tamisemi anayeshughulikia Elimu.

Kabla ya uteuzi huo Mweli alihudumu kama mkurugenzi wa mipango katika wizara ya Katiba na Sheria.

Hashim Abdallah Komba naye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea. Kabla ya Uteuzi huo Komba alikuwa akihudumu kama katibu tawala mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ilioachwa na Rukia Muwango ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Vilevile Rais Magufuli alimteua Hassan Abbas Rungwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea. Anachukua mahala pake bakari Mohammed Bakari ambaye ameondolewa na huenda akapatiwa kazi nyengine.

Rais Magufuli alimpongeza nampongeza Hussein Katanga ambaye amemteua kuwa Balozi na alisema ameamua kuwa aende akamsaidie kwenye kazi maalumu kwenye nchi fulani na kwamaba atakwenda kumwakilisha vizuri kule

Alisema Katanga ametimiza kazi zake vizuri katika nafasi zake zote na kwamba aameamua umchukua akamwakilishe katika nchi fulani na kwamba anajua italeta impact (matokeo) hivyo kumshukuru kwa utendaji wake

Alisema Kabunduguri ni mtaalamu wa reforms (mabadiliko) na kwamba anaamini atakwenda kumsaidia vizuri kwenye mahakama kwa kuwa rekodi yake ni nzuri.

Alisema mahakama inafanya kazi nzuri na wamefanya mabadiliko mengi na kuifanya mahakama kuwa kimbilio pekee la haki kwa wananchi wanyonge..

Alisema Naibu Katibu Mkuu alikuwa wizara ya elimu ambapo amefanya kazi nzuri akaenda mambo ya nje, lakini sasa wakaona aendee kuwasaidia kwenye Tamisemi katika upande wa elimu na kumtaka akasimamie vizuri na kutatua kero za walimu, shule, madarasa na maabara.

Alimtaka akaangalie kero za walimu hasa madai yao na promosheni zao kwamba hakuna sababu za walimu kuendelea kulalamika na watendaji wa wizara kutopata stahiki zao kwa wakati wakati yeye akiwepo, hivyo akashirikiane na waziri wa Tamisemi na makatibu wakuu wenzake.

Aliwapongeza wateule hao na kwamba kwa kuteuliwa kwao na ni matumaini watakwenda kutimiza wajibu wao vizuri na wakakumbuke miiko waliyoiapa katika kuapishwa kwao ili wakaitimize kwa ajili ya wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here