27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli azua minong’ono Kenya

John Magufuli
John Magufuli

NAIROBI, KENYA

SERIKALI ya Kenya imepuuza kutokuwapo kwa Rais wa Tanzania, John Magufuli wakati wa mkutano wa kimataifa uliomalizika hivi karibuni nchini hapa.

Hilo limetokana na kuenea kwa minong’ono na wasiwasi miongoni mwa Wakenya juu ya dhamira yake ya utangamano wa kikanda.

Wakenya wengi walitarajia Magufuli kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na uwapo wa Japan kupitia mpango wake wa Ushirikiano na Maendeleo ya Afrika (Ticad), angehudhuria mkutano huo.

Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed, alipuza madai hayo  akisema Rais Magufuli alituma mwakilishi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

“Si yeye pekee ambaye hakuhudhuria mkutano. Kusema kweli, aliwakilishwa vyema na hivyo hakuna haja ya kuhofia. Tanzania na Kenya zina uhusiano mzuri, tuache kujikita kuwaza mabaya,” Mohamed alisema katika mahojiano kwa njia ya simu.

Tangu aingie madarakani Oktoba mwaka jana, Magufuli ametembelea Uganda na Rwanda pekee.

Tofauti na mtangulizi wake Jakaya Kikwete, ambaye alijulikana kwa kusafiri nje, Rais Magufuli amejikita katika masuala ya nyumbani, akipambana na ufisadi katika utumishi wa umma.

Safari yake ya kwanza ya kigeni ilikuwa Rwanda Aprili, mwaka huu kuadhimisha miaka 22 ya mauaji ya kimbari na mwezi uliofuata alihudhuria kuapishwa kwa muhula wa tano kwa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Lakini pia Magufuli hakuhudhuria mikutano kadhaa ya kimataifa ukiwamo wa Taasisi ya Kimataifa ya Biashara (WTO) jijini Nairobi, Desemba mwaka jana.

Mingine ni Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa Januari mwaka huu, Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (Unctad) jijini Nairobi mwezi uliopita pamoja na mkutano wa kilele wa AU mjini Kigali.

Mkutano wa Ticad ulielezwa kwamba hatimaye utamleta Kenya, hasa pia kutokana na ahadi ya Japan ya miradi mikubwa ya miundombinu.

Wakati wa ziara yake Rwanda, Rais Magufuli pia alishuhudia kufunguliwa kwa Daraja la Kimataifa Rusumo linalounganisha Tanzania na Rwanda na ambalo ujenzi wake ulifadhiliwa na Japan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles