23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Magufuli azifagilia nchi za Nordic kusaidia ukombozi Afrika

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais Dk. John Magufuli amezipongeza nchi za Nordic kutokana na msaada wake mkubwa katika kusaidia harakati za ukombozi kwenye nchi mbalimbali hususani kusini mwa Afrika.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ijumaa Novemba 8, katika ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje na nchi za Nordic ambapo Tanzania ndiyo mwenyeji wa mkutano huo uliozikutanisha nchi 34 zikiwamo za Nordic.

“Kama mnavyofahamu Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa harakati za ukombozi ambapo kulikuwa na kambi nyingi za wakimbizi hivyo tunafahamu mchango mkubwa wa Nordic ikiwamo ujenzi wa Chuo cha Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini cha Solomon Malangu Freedom College (Somapco), kilichojengwa mwaka 1975 mkoani Morogoro.

“Ikumbukwe kuwa nyakati hizo haikuwa rahisi kwa mataifa ya Ulaya kuja kuunga mkono jitihada za ukombozi kwa nchi za Afrika, lakini marafiki zetu wa nchi za Nordic walikuja, na huu ndiyo upekee wa nchi za Nordic ahsanteni sana,” amesema Rais Magufuli.

Amesema hata baada ya kusimamia harakati za kupigania uhuru nchi za Nordic zimeendelea kuwa washirika wa maendeleo wa nchi za Afrika, ambapo wameshirikiana katika nyanja nyingi ikiwamo afya, elimu, kilimo, sayansi, kilimo, amani na usalama.

Aidha, amesema nchi hizo hususani Tanzania, imenufaika na miradi mingi ya nchi za Nordic ikiwamo  Kituo cha Elimu Kibaha (Kibaha Education Centre) na Kituo cha Utafiti cha Kilimo Uyole.

“Nchi za Nordic zilitusaidia kujenga vyuo vya ufundi na pia kwenye kampeni za kufuta ujinga (Illiteracy Campaign  Programme), iliyotekelezwa miaka ya ‘70 na kuiwezesha Tanzania kufuta ujinga kwa ailimia 98 na hivyo kuwa nchi za kwanza Afrika kufikia kiwango hicho, sina hakika kama kiwango hicho kimeshafikiwa na nchi nyingine.

“Leo nataka niwashukuru kwa sababu na mimi ni product ya wanufaika wa nchi za Nordic kwa sababu digrii yangu ya kwanza kwa miaka yote mitatu nikifabnya thesis na research zilitolewa fedha na nchi ya Norway kwa kupiftia Shirika la Norad kwa hiyo na mimi nawashukuru.

“Kwa kuzingatia hayo yote napenda nitoe shukrani zangu za dhati kwa kuendelea kushirikiana na nchi za Afrika na tunawaomba mawaziri wetu wa mambo ya nje mfikishe salamu zetu kwa nchi zenu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,712FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles