24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli awatoa hofu Watanzania Stiegler’s Gorge haitaharibu mazingira

Anna Potinus, Dares Salaam

Rais John Magufuli amewatoa hofu Watanzania wanaoamini kuwa mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge wa Bonde la Mto Rufiji utasababisha uharibifu wa mazingira kwani ukweli ni kwamba utasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira

Ameyasema hayo leo Jumatano Desemba 12, katika hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi huo na Serikali ya Misri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema mradi huo ni rafiki wa mazingira.

“Kuna watu wanasema kuwa mradi huu utaharibu mazingira lakini nataka niwahakikishie kuwa mradi huu utasaidia kutunza mazingira kwani utapunguza ukataji wa miti kwa asilimia kubwa,” amesema.

Aidha amesema kuwa baada ya mradi huo kukamilika utaokoa miti mingi inayokatwa kwa ajili ya matumizi ya mkaa ambapo jijini Dar es Salaam ndiyo inayoongoza kwa kuwa na matumizi makubwa ya mkaa.

“Tuna imani kubwa wananchi wengi wataachana na matumizi ya mkaa na kuni na kutumia umeme kwa bei nafuu na niseme tu kwamba Watanzania ni watunzaji wazuri wa mazingira,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles