30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli awapa polisi ofisi Dodoma

Mwandishi Wetu, Dodoma

Rais Dk. John Magufuli, amewapa ofisi jeshi la polisi jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya jeshi hilo na serikali kuhamia jijini humo.

Akizungumza katika uzinduzi wa ujenzi wa nyumba za polisi eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo Ijumaa Novemba 22, amesema anawakabidhi jengo la ghorofa nne lililokuwa linatumiwa na Uwasa ambapo yatakuwa makao makuu ya jeshi hilo.

“IGP nimefurahi umesema umehamia hapa Dodoma, ningeshangaa kuona mimi nimehamia hapa wewe bado hujahamia, ningeteua IGP wangu wa hapa Dodoma.

“Lakini kwa sababu umewahi umehamia hapa nakushukuru na kwa sababu umehamia kufanya hivyo kwa sababu askari hasubiri nyumba nimeamua kuwapa zawadi, siyo hela mimi sitoagi hela nimeamua kwa vile mmeshatekeleza wito wa kuhamia hapa na sitaki kujua mmehamia wapi inawezekana  mnakaa kwenye miembe kwenye nini, lakini jukumu lenu mmelifanya la kuhamia hapa nimewamua kuwapa jengo moja kubwa lenye ghorofa nne lilikouwa linatumiwa na Uwasa.

“Sasa ndiyo yatakuwa Makao Makuu ya Polisi na ninakupa picha zenyewe ni matumaini yangu leo nitaona makao maku  yapolisi kwenye jengo hilo,” amesema Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli amesema serikali imeshahamia Dodoma hakuna lugha nyingine kwamba watahamia, hapa ndiyo makao makuu hakuna jingine na watabanana hapa hapa kwa wagogo hakuna namna.

“Dodoma inapendeza, Dodoma inavutia. Na katika miaka michache ijayo jiji hili litaipita hata jiji la Dar es Salaam na majiji mengine,”- amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles