30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Magufuli ateua ma-dc wawili

Mwandishi Wetu- Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli, ameteua wakuu wa wilaya wawili kuziba nafasi zilizoachwa na waliokuwapo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo habari na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Dar es Salaam jana, ilisema katika uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua mtangazaji mkongwe wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Bakari Msulwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, akichukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.

Msulwa alianza kazi mwaka 1989, alipojiunga Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na alianza kazi rasmi mwaka 1990.

Alifanya kazi Iliyokuwa Idhaa ya Nje ya RTD, ‘External Service, Idhaa ya Taifa na baadaye Idhaa ya Biashara.

Pia Rais Magufuli amemeteua Kamishna Msaidizi wa Polisi, Edward Balele kuwa MKuu wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, akichukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Iddi Kimata ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa MKoa wa Arusha mwisho mwa wiki.

Juzi pia, Rais alimteua Kenasi Kihongosi aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Iringa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha akichukua nafasi ya Gabriel Daqarro. Mwishoni wiki Rais Magufuli, alitengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwa kile kilichoelezwa kutokua na uhusiano mzuri na watendaji wenzake. Viongozi hao wanatarajia kuapishwa leo Ikullu, Dar es Salaam

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,854FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles