25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli: ATCL kuweni makini lugha mnazotumia kwa wateja

Anna Potinus

Rais Dk. John Magufuli ameutaka uongozi na watumishi wa Shirika la Ndege nchini (ATCL), kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kuachana na tabia ya kutoa lugha mbaya kwa wateja na badala yake kuwahudumia kama wafalme kwakuwa wao ndio waajiri wao.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Oktoba 26, alipokuwa akipokea ndege mpya Boeing 787-8 Dreamliner ya Air Tanzania Jijini Dar es Salaam.

“Nitoe wito kwa uongozi na watumishi wa ATCL tekelezeni majukumu yenu kwa ufanisi na weledi, ninafahamu kuna malalamiko mengi yanayotolewa na baadhi ya wateja kuhusu ucheleweshwaji wa safari na kuambiwa ndege imejaa ilihali bado kuna viti viko wazi na wakati mwingine lugha zinazotolewa na maofisa sio nzuri hivyo ninaomba mjirekebishe nisingependa kusikia malalamiko hayo tena kwani wateja ndio waajiri wenu hivyo ni lazima muwahudumie kama wafalme,”.

“Endeleeni na makakati wenu wa kupanua mtandao wa safari zenu ndani na nje ya nchi na kwenye hili sina tatizo na muendelee kushirikiana na bodi ya utalii na mashirika mengine kwaajili ya kutangaza kazi nzuri na maeneo mazuri ya utalii katika nchi yetu,” amesema Rais Magufuli.

Amesema ndege nyingine nne zinatarajiwa kuwasili nchini kwa nyakati tofauti ambapo moja ya masafa mafupi itawasili Novemba mwaka huu, nyingine itawasili Juni mwaka 2020 na nyingine mbili zinatarajiwa kuwasili kati ya Juni na Julai 2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles