30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Magufuli atakiwa kushughulikia Z’bar

Tanzania's Works Minister John Magufuli addresses delegates after the ruling party CCM elected him as the presidential candidate for the October 25 election in the capital DodomaNA OSCAR ASSENGA, TANGA

RAIS Dk. John Magufuli, ameombwa kutoa nafasi kubwa zaidi ya mazungumzo kuhusu mgogoro wa kisiasa Zanzibar, ili kujali na kuthamini uamuzi wa wananchi walioufanya wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Ombi hilo lilitolewa juzi na Mbunge wa Viti Maalumu Wilaya ya Magharibi A Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Raisa Mussa wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.

Mgogoro huo umekuja  baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi huo kwa madai kulikuwa na dosari nyingi.

Raisa alisema hakuna sababu ya kuipeleka Zanzibar kwenye machafuko na kumtaka Rais Magufuli achukue hatua haraka.

“Zanzibar itakapoingia katika machafuko, atakayelaumiwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenyewe ndiyo iliyobeba dhamana kubwa ya kupatikana suluhu ya tatizo hili,” alisema.

Alisema anashangazwa na Tanzania kuwa mstari wa mbele kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi nyingine, ikiwamo Burundi wakati  Zanzibar bado kunafukuta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles