Magufuli ataka mahakama zinazotembea ziongezwe kushughulikia wajane

0
690

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais John Magufuli amezindua Mahakama inayotembea (Mobile Court), huku akisisitiza yaongezwe magari mengine zaidi kushughulikia kesi za mirathi kwa ajili ya wajane.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akihutubia wanasheria katika kilele cha siku ya Sheria iliyofanyika leo Februari 6, jijini Dar es Salaam.

“Nendeni mkatende haki, kuna watu wanalalamika sana hasa suala la mirathi mkalishughulikie, kuna wajane wanapata shida sana.

“Mirathi inachukua miaka sita, unashangaa inakuwaje, naomba mkaliangalie hili, ili wajane hawa wapate haki.

“Ningefurahi kungekuwa na gari linaloshughulikia mirathi kwa kina mama wajane na hakimu atakayekuwa mule awe mwanamamama wanateseka mno, yaongezwe hata magari mengine mawili,” amesema Rais Magufuli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here