22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Magufuli amwagiza Mkurugenzi Dodoma kuwalipa bilioni tatu waliopisha ujenzi Makao Makuu JKT

Anna Potinus

Rais John Magufuli amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma kuwalipa fidia ya Sh bilioni 3.399 wakazi waliopisha ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) katika eneo la Kikombo jijini humo.

Aidha amewataka wananchi wanaostahili kulipwa fidia kuacha kuwasikiliza matapeli wanaowadanganya kuwa ndio wenyeviti wanaosimamia mafao yao na badala yake wahakikisha wanaenda kuchukua fedha zao ifikapo Desemba Mosi mwaka huu kwani mtetezi wao ni serikali na sio mtu mwingine yeyote.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Novemba 25, katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Makao makuu ya JWTZ.

“Kwasababu jiji la Dododoma liko pale kwa kujibu wa sheria na ninafurahi kwamba Mkurugenzi ambaye ni kijana amekuwa akiongoza kwenye makusanyo katika jiji hili ninatoa maelekezo leo kwa Mkurugenzi wa jiji achukue milioni 3.399 kuanzia Desemba Mosi mwaka huu aanze kuwalipa fidia wananchi wa hapa bila kuwapunja.

“Ninatoa wito kwa wananchi wanaopaswa kulipwa fidia msianze kubadilisha hizo fidia maana ninafahamu kuna matapeli ambao wanapita kwenye maeneo yenu wakijiita kuwa ndio wenyeviti wa kutete fidia embu achaneni nao maana mtetezi ni serikali wala wasije wakawadanganya kwani wa kufanya hivyo mnajichelewesha.

Ameongeza kuwa kwa wale watakaojichelewesha kuchukua fidia hiyo ninajua wanajeshi wakishaingia rasmi katika eneo hilo itabidi waende kuwaomba wao mwenyewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles