28.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Magufuli amtuma Makonda kuwatia moyo wachezaji Taifa Stars Misri

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Rais John Magufuli amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda kwenda nchini Misri kwenye mashindano ya kuwania Kombe la Afrika (AFCON) na kuwatia moyo wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars)

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumanne Juni 25, wakati akizindua mitambo ya gesi ya Kampuni ya Taifa Gas Ltd, jijini Dar es Salaam.

“Makonda umesema unataka kwenda Misri, nakutuma nenda hata leo na kawaambie wachezaji wasikate tamaa kushinda kwao ndiyo ushindi wa Tanzania na hata wakishindwa pia tunashindwa wote kufungwa magoli mawili kusiwakatishe tamaa kwa sababu ni mwanzo siyo mbaya.

“Mwanzo wa Taifa Stars siyo mbaya, kwanza wamefungwa tugoli tuwili tu na timu kubwa kama ile yenye wachezaji wengi Ulaya, nina imani watafanya vizuri tuendelee kuwaombea na kuwashingilia, ” amesema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,085FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles