24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli ampa rungu Sirro

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro, kutowapeleka Makao Makuu wa jeshi hilo maofisa wanaoshindwa kufanya vizuri katika vituo vyao.

Akizungumza baada ya kuwaapisha mawaziri wawili Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Machi 4, Rais Magufuli pia amemtaka Sirro kutoogopa kuleta majina ya watu ambao wanatakiwa kupunguziwa vyeo.

“Nakuomba IGP, watu ambao wanaoshindwa ‘kuperfom’ wasiwe wanapelekwa makao makuu, mpeleke hata akawe ‘Senior RPC’ chini huko.

“Pia usiogope kuleta makamishna ambao unataka tuwapunguze hata nyota zao wala usisite kwa sababu tumezoea kutoa nyota, tu sasa tutazichukua…” amesema Rais Magufuli.

Aidha, akizungumzia kuhusu rushwa, amesema watu wasitegemee kupata vyeo kwa sababu ya rushwa bali atapata cheo kwa sababu ya utendaji wake.

“Tumekaa Mwanza kule kuna ushahidi wa kutosha kwamba wale polisi walihusika kusindikiza ile dhahabu na wakahongwa mamilioni ya fedha.

“Inapofikia wanajeshi wanahongwa mamilioni ya fedha kunakuwa na hitilafu, niwaombe makamishna tujenge jeshi la polisi kama lilivyoanzishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, wale wachache wanaolichafua waonyeni ikishindikina kuonywa shusha,” amesema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles