22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Magufuli ampa kibarua kizito Kichere; “Ofisi ya CAG siyo ‘clean’ kaisafishe”

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

 Rais Dk. John Magufuli, amesema Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), siyo safi kama watu wanavyodhani bali kuna uchafu mwingi wakiwamo watumishi wasio waaminifu.

“Ofisi ya CAG siyo clean (safi) kama mnavyofikiria, sasa nenda ukachambue ukapange position (nafasi) za watu wako ili mauchafu uchafu haya ukayasafishe,” amesema Rais Magufuli wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua mwishoni mwa wiki akiwamo CAG Charles Kichere, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Novemba 4.

Pamoja na mambo mengine amemtaka CAG Kichere kutojifanya kuwa sehemu ya mhimili wakati yeye ni mtumishi hivyo akafanye kazi na maagizo anayopewa na mihimili mbalimbali kama Bunge na Mahakama bila kubishana wala kuonea watu.

“CAG mpya, nakutakia kazi njema. Usije ukaenda huko ukajifanya na wewe ni mhimili, mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa kuna Mahakama, kuna Bunge na sisi wengine wa serikali.

“Na nataka nikueleze kabisa hapa mapema, katiba inazungumza unaweza ukakaa miaka yako hiyo mitano na unaweza kukaa hata mwaka mmoja kwa sababu taratibu zipo na zinafanywa na rais, lakini sikutishi wewe nenda ukachape kazi.

“Duniani humu huwezi ukapewa mamlaka ya kuteua halafu usiwe na  mamlaka ya kutengua ukishindwa hivyo hufai kuwa rais na hufai kuwa kingozi.

“Mwenzako aliyekuwepo amemaliza kipindi chake cha miaka mitano na kinaisha leo usiku nafikiri saa sita, kwa hiyo kuanzia kesho uende pale ofisini  ukaanze kufanya kazi ukamtangulize Mungu, ukatimize wajibu wako, ukayatoe mauchafu uchafu yote yaliyopo hapo mengine watakueleza wizara ya fedha ambayo wanayafahamu vizuri zaidi.

“Lakini pia kasimamie hiyo ofisi, kuna baadhi ya watendaji wako utakwenda kuwakuta kule, wanapotumwa kwenda kukagua kwenye balozi wanalipwa fedha hapa na wakifika kule napo wanaomba fedha, sasa sitaki nikutajie majina yao nenda mwenyewe ukachambue kwenye ofisi hii.

“Lakini pia una heshima, unatolewa kwenye ukamishna wa TRA hukusema neno ukaenda kufanya kazi huko, hukutamka neno. Wapo wengine ukiwateua wanafikiri ni nafasi zao, unampa u-DC ukimtoa anaanza kulalamika, sasa mbona hukulalamika wakati nikikuteua kwa hiyo kafanye kazi,” amesema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles