23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli ‘alivyowasuprise’ askari, wafungwa Butimba

Anna Potinus

Rais John Magufuli amewafanyia ‘surprise’ mahabusu na wafungwa wa gereza la Butimba kwa kuwapa ng’ombe watatu na magunia 15 ya mchele ili waweze kusheherekea na kula kwa pamoja na askari polisi wa gereza hilo.

Ametoa ahadi hiyo leo Jumanne Julai 16, alipotembelea gereza hilo mkoani Mwanza ambapo alipata fursa ya kusikiliza baadhi ya kero zinazowakumba mahabusu na wafungwa ambapo amewataka kuacha kufanya makosa yanayowamuiza watu waliopo uraiani.

“Serikali yangu haipendi watu wafungwe lakini na ninyi wafungwa msifanye makosa ambayo yamewaumiza watu waliopo uraiani, wapo mlioua, wanaotuhumiwa kwa ugaidi na wengine wengi waliofanya mambo makubwa tu,” amesema.

“Nitatoa ng’ombe watatu na magunia 15 ya mchele na hao ng’ombe wachinjiwe na hawa wafungwa wenyewe halafu wapike kasha mle ninyi maaskari na vijana hawa kwani kula kwa pamoja kunajenga upendo wa Mungu na upendo wa kweli,” amesema.

Aidha rais Magufuli amewataka wafungwa na mahabusu hao kuendelea kumuomba Mungu awasamehe makosa yao kwakua hakuna dhambi kubwa wala ndogo na kwamba dhambi zote zinasameheka,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles