24.1 C
Dar es Salaam
Saturday, September 21, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli aitaka Zimbabwe kufutiwa vikwazo vya kiuchumi

Anna Potinus

Rais Dk. John Magufuli ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kuiondolea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Zimbabwe ambapo amesema kuwa vikwazo hivyo vimelemaza uchumi wa taifa hilo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Agosti 17, alipokuwa akihutubia wakuu wa nchi Wanachama Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa jumuiya hiyo na Rais wa Namibia, Dk Hage Geingob ambapo ataingoza kwa kipindi cha mwaka mmoja.

“Vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe vinaathiri ushirikiano wake katika Jumuiya ya jumuiya hii ya SADC hivyo ninomba nchi hiyo ipewe nafasi ya pili kwa sababu ina utawala mpya,” amesema.

Zimbabwe iliwekewa vikwazo na mataifa ya Magharibi kutokana na hatua ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe, kuchukua kwa lazima ardhi ya wahamiaji wenye asili ya kizungu.

Aidha Rais Magufuli ameapa kuhakikisha amani inadumishwa ili kukwamua uchumi wa mataifa wanachama wa SADC.

“Tunaahidi kushirikiana na nchi zote wanachama wa SADC kuhakikisha kupitia mkutano huu ndoto na mawazo ya Baba yetu wa Taifa pamoja na viongozi wengine waanzilishi wa Jumuiya hii yanaendelea kutekelezwa kwa vitendo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles