23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli aitaka NFRA kuuza vyakula vilivyopo katika maghala

Betsheba Wambura, Dar es Salaam

Rais Dk. John Magufuli amewataka Wakala  wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuacha kuweka vyakula katika maghala ilihali havitumiki na badala yake waviuze kwa mashirika na taasisi mbalimbali wanaovihitaji na kisha wapeleke pesa hzi kwa wakulima ili kutengeneza mzunguko mzuri wa kilimo hapa nchini.

Akizungumza leo Ijumaa Januari 4, baada ya kushuhudia utiaji wa saini wa mkataba  wa makubaliano ya  mauziano ya mahindi kati ya NFRA na Shirika la Chakula Duniani (WFP) katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Saalaa ambao utagaharimu Sh. Bilioni 21.

Rais Magufuli amesema NFRA walikuwa na shida, kila mwaka serikali inatenga fedha kwa ajili ya kununua chakula kwa kutegemea kitasaidia wakati wa njaa lakini matokeo yake njaa hakuna na vyakula havijulikani vinapoenda.

“NFRA  ilikuwa ni tatizo kwasababu kila mwaka serikali inatenga bajeti tani 250 za mazao zinanunuliwa halafu yanapotelea kusikojulikana, kwasababu tuna ipindi kirefu hatujapata njaa, ila ukweli ni kwamba yalikuwa yanauzwa tena kwa bei ya chini.

“NFRA  mbadilike msitegemee kila mwaka ntakuwa natoa fedha nawapa, unatoa pesa mwaka huu mwakani unatoa tena hakuna ‘return’ yoyote na wala hakuna njaa, mwaka huu zilitengwa bilioni 90 nikakataa nikawapa bilioni 19 niiikuwa nawatega tu ila kwakweli mnahitaji kubadilika, “ amesema.

Amesema uwekwaji wa saini hiyo ni hatua muhimu kwani ni fursa kwa wakulima wa Tanzania kuuza mazao yao kwa WFP,wakati mazao yakiuzwa kwa bei ya chini huko mikoani na mengine kukosa masoko lakini sasa soko la uhakika limepatikana.

Aidha amelishukuru shirika hilo kwa kununua chakula hapa nchi na kuzitaka mamlaka za Shirika la Reli (TRC), Mamlaka ya Bandari (TPA), Mamlaka ya Mapato(TRA), Wakala wa Barabara (TANROADS) na Jeshi la Polisi kutoweka vikwazo kwa WFP wanapotaka kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles