26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mageuzi makubwa ya kilimo ndio yatakayowainua wananchi Kibakwe-Simbachawene

Na Mwandishi Wetu, Kibakwe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene amehimiza watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kufanya mageuzi makubwa ya kilimo kwa kuwekeza katika miradi ya kimkakati itakayoongeza uzalishaji katika sekta hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene akikagua maendeleo ya ujenzi katika kituo cha afya Ipera kilichotengewa na Serikali Sh million 500 katilka jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.

“Lazima tuwekeze fedha kwenye miundo mbinu ya uzalishaji wa kilimo, wataalam wa kilimo wanaojengewa uwezo na wizara ya kilimo, wafanye kilimo shambani nawatumie maarifa waliyopata kwa kushirikisha wakulima,” amesema Simbachawene.

Simbachawene ameyasema hayo juzi alipofanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kinusi Jimbo la Kibakwe katika Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.

“Kata ya Malolo na kata Ipera ni eneo ambalo limejikita katika kilimo cha umwagiliaji, Halmashauri itizame namna ya kuimarisha miundo mbinu ya maji ili maji yasipot,’ alisema Simbachawene.

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika bajeti yake ya 2022/23 imejikita katika maeneo ya uzalishaji, bajeti ya kilimo imeongezwa kutoka Sh billion 200 mpaka Sh billion 900, hivyo fedha nyingi zitaletwa kijijini katika miradi ya kimkakati ya kilimo.

“Serikali imeleta pembejeo za ruzuku, baadhi ya gharama zitalipwa ili mwananchi wapate pembejeo kwa bei nafuu, ni lazima maafisa kilimo wajue hiyo mifumo ili waweze kuwasaidia wakulima,” amesema Simbachawene.

Awali, diwani wa kata ya Ipera, Festo Myuguye ameomba serikali kupimia wananchi maeneo yao na viwanja vyao, ili wananchi waweze kupata fursa ya kutumia hati za viwanja vyao kupata mikopo.

“Tunaomba pia serikali itusaidie kujenga miundo mbinu ya maji katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo ili kuwafikia watu wengi, miundo mbinu iliyopo ilijengwa kabla ya Kijiji kuwa kikubwa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles