28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

MAGEREZA NCHINI YANA MSONGAMANO MKUBWA WA WAFUNGWA – WAZIRI

NA RAMADHAN HASSAN, Dodoma


 

SERIKALI imekiri kukabiliwa na changamoto kubwa ya msongamano wa wafungwa nchini.

Imesema wakati wafungwa waliopo magerezani ni  40,000 uwezo wake ni wafungwa  wasiozidi 30,000 hivyo kuzidiwa na wafungwa 10,000.

Hayo yalielezwa  bungeni jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni alipojibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Molel (Chadema).

Katika swali lake ,Mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kupunguza mahabusu  miundombinu iweze kumudu.

Masauni alikiri kuwapo   tatizo la msongamano wa wafungwa ambako waliopo kwa sasa ni 40,000 wakati uwezo ni wafungwa 30,000.

Naye Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema)   amehoji Serikali inachukua hatua gani kupunguza msongamano wa wafungwa nchini.

Akiuliza swali la nyongeza  bungeni jana, Msigwa alisema kuwa Gereza la Segerea, Dar es Salaam limezidiwa na mahabausu.

Alisema gereza hilo  lina uwezo wa kuchukua mahabusu 700, lakini waliopo kwa sasa ni mahabusu na wafungwa  2400.

“Ukienda katika magereza yetu kuna msongamano mkubwa   kwa mfano Gereza la Segerea ambalo nililipitia juzi lina uwezo wa kuchukua mahabusu 700 lakini sasa hivi lina mahabusu na wafungwa 2400.

“Wanalazimika watu kulala upande mmoja mmoja kwa zamu baada ya muda inapigwa ‘alarm’ kisha mnageukia upande mwingine.

“Huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu na watoto wengi wapo   chini ya umri wanatakiwa waende shule.

“Ni kwa nini Serikali imekuwa ikipeleka wanasheria kutetea kesi za Serikali ambao wamekuwa wakilazimisha wale ambao wanaweza kupata dhamana waende kukaa mahabusu kama ambavyo kesi zetu zilikuwa zina dhamana.

“Lakini mawakili wa Serikali wamekuwa wakilazimisha tuende kule tukaongeze msongamano?” aliuliza Msigwa.

Akijibu, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William ole Nasha, alisema kuwekwa ndani kwa muda mrefu kwa mahabusu hakumaanishi Serikali haitaki kesi hizo zimalizike haraka.

“Sababu za msingi ni sababu ya usalama wao.

“Wakienda nje wanaweza wakapata matatizo ikiwamo Serikali kuwalinda pili kuna watuhumiwa wakitoka nje wataenda kuharibu ushahidi,”alisema.

Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko (Chadema) katika swali lake la nyongeza, aliitaka serikali iwaachie kina mama ambao wamefungwa huku wakiwa wanaumwa.

“Nimekuwa Segerea Mheshimiwa Spika, kule kuna wamama wamefungwa wanadaiwa mathalani Sh 150,000 lakini amefungwa miezi sita kwa gharama ambazo amezitoa Naibu Waziri zinavuka mpaka Sh 200,000.

“Kwa nini Serikali isitumie busara kwa kina mama ambao wengine wana watoto wachanga wanafungwa kwa kesi ya Sh 100,000 mpaka Sh 200,000 na Serikali inatumia gharama kubwa katika gharama za chakul?”alihoji Matiko.

Akijibu swali hilo, ole Nasha alisema suala hilo ni la  sheria hivyo kama Mbunge anaona hoja hiyo inamashiko apeleke hoja binafsi bungeni.

Akiongezea majibu,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba, alisema   wahalifu hawawezi kuachwa nje kwa kuogopa magereza kujaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles