20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

MAGEREZA: LULU ‘AMETOKA’ KWA MSAMAHA WA RAIS

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Msanii nyota wa Filamu, Elizabeth Michael maarufu Lulu, ameachiwa huru kwa msamaha wa Rais John Magufuli, alioutoa kwa wafungwa katika Sikukuu ya Muungano Aprili 26, mwaka huu.

Hata hivyo, msamaha wa rais kwa msanii huyo ambaye ameachiwa Jumamosi wiki iliyopita, ni kubadilishiwa au kupunguziwa adhabu kutoka kifungo cha miaka miwili alichokuwa akitumikia hadi kifungo cha nje ambacho atamaliza Novemba 12, mwaka huu.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Jumatatu Mei 14,  Naibu Kamishna wa Magereza, Augustino Mboje amesema Magereza ilipokea amri kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,  kwamba mfungwa huyo amebadilishiwa adhabu hivyo wamwachie huru.

“Ieleweke bado ni mfungwa wetu na angeendelea kukaa gerezani hadi Novemba 12, mwaka huu ila hiki kifungo kimepunguzwa kwa msamaha wa rais bila msamaha wa rais ambaye amempunguzia moja ya sita ya adhabu ya kifungo chake, ilikuwa atoke machi 12, mwaka 2019.

“Kwa hiyo bado ni mfungwa kwa mujibu wa Sheria Community Service Namba sita ya 2002 ambayo inaruhusu mtu kutoka akawa na kifungo cha nje yaani kifungo cha huduma za jamii, hii ina maana atapangiwa kazi wilayani, sijui wilaya gani, na atapangiwa kazi kwa masaa fulani kwa siku tano. Hatakuwa chini yetu yetu kwa masharti ya sheria hiyo,” amesema.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili Novemba mwaka jana, kwa kosa la kumuua bila kukusudia mpenzi wake, Steven Kanumba ambaye pia ni muigizaji mwenzake, Aprili 7, mwaka 2012.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles