22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Magari yanayozoa taka yaongeze siku za kazi

AVELINE KITOMARY

UTABIRI wa hali ya hewa unaonesha kuwa mvua zitaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini, hii ni baada ya kuchelewa kwa msimu wa masika kulikosababishwa na kimbunga Keneth.

Mvua hizi zimesababisha baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam kujaa takataka kutokana na kutokuzolewa kwa wakati.

Hii ni hatari kwani kuna takataka zingine zinasombwa na maji nyingine huishia barabarani au kwenye makazi ya watu. 

Uzoaji wa taka maeneo ya Dar es Salaam, umekuwa ukilalamikiwa mara nyingi na wakazi wa jiji hili hasa wafanyabishara, lakini bado suluhisho sahihi la kuzolewa kwa wakati halijapatikana. 

Hali hii imegeuka kero kwa wananchi, jiji limekuwa chafu hali ambayo inaweza kusababisha milipuko ya magonjwa kama kipindundu.

Maeneo hasa ya barabarani, katika mitaa mbalimbali ndiko uchafu unakokusanywa ili kusubiri gari, kwa bahati mbaya magari ya kuzolea taka hayafiki kwa wakati hivyo kuzifanya ziharibu mazingira ya sehemu husika.

Kuna baadhi ya maeneo taka huzolewa mara moja, kwa wiki huku uzalishaji wake ukiwa ni mkubwa na hivyo wakati mwingine huleta harufu na mbaya mtaani. 

Hali ni mbaya zaidi katika masoko ambayo miundombinu yake ni mibovu. Mfano wa masoko hayo ni Buguruni, Ilala na hata soko la Mabibo.

Ukienda sokoni katika kipindi hichi cha mvua, utakutana na harufu ya ajabu inayosababishwa na uchafu wa mazingira.

Masoko mengine yanayochinja kuku harufu huwa kali zaidi kwa sababu ya uchafu hasa kwa kipindi hiki.

Naishauri mamlaka husika za uzoaji taka kujitahidi kuzoa takataka zilizopo maeneo mbalimbali ya jiji kwa wakati ili wananchi waweze kuepukana na kero hiyo.

Magari na vifaa vya kuzolea taka viongezwe ili kuweza kurahisisha zoezi hili, hii itasaidi mitaa na hata masoko kuwa masafi. 

Pia wananchi wajitahidi kutotupa taka hovyo katika mitaa yao, badala yake wakusanye sehemu moja hadi gari maalumu litakapofika kuzichukua, hii ni kwa faida ya wananchi wenyewe na si vinginevyo, kwani yanapotokea magojwa ya mlipuko wananchi wa hali ya chini ndio huwa wa kwanza kuathirika kutokana na mazingira wanayoishi.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles