23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MAFUTA YA NAZI YATAJWA KUWA HATARI KWA AFYA YA BINADAMU

FREIBURG, Ujerumani


UTAFITI mpya umebaini kwamba,  mafuta ya nazi ni ‘sumu halisi’ na si tiba kama ilivyodhaniwa na watu wengi na hivyo kutajwa kuwa ni hatari kwa afya ya binadamu.

Tahadhari hiyo ambayo imezua  maswali mengi imetolewa na Profesa Karin Michels, kutoka kitengo kinachoshughulika  na magonjwa  ya binadamu katika Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani, wakati akitoa  hotuba yake mjini Freiburg nchini hapa  ambayo baadaye iliwekwa katika mtandao wa You Tube.

Katika hotuba hiyo ambayo inadaiwa kutazamwa na watu zaidi ya milioni moja, Profesa Michels, alisema kwamba  mafuta ya nazi ni miongoni mwa vyakula vibaya zaidi kula.

“Chakula hicho kina mafuta mengi ambayo yanaweza kusababisha madhara katika viungo vya ndani ya mwanadamu kama inavyoelezwa kuhusu nyama ya nguruwe inavyosababisha saratani, ama kwamba mvinyo mwekundu si mzuri kwa afya ya mwanadamu,” alisema Profesa huyo katika hotuba yake hiyo.

“Ni wiki iliyopita tulipogundua kwamba, licha ya miaka kadhaa kuambiwa kwamba vyakula visivyo na madini ya kabohydrayte vinaweza kupunguza miaka ya maisha yako,” aliongeza.

Victoria Taylor ambaye ni Ofisa Mwandamizi kutoka kitengo cha matatizo ya moyo nchini Uingereza kuhusu lishe bora, aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza kwamba, Profesa Michel yuko sawa licha ya kampeni kubwa ya kukuza mafuta hayo.

Alisema kwamba, mafuta ya nazi yamejaa koresta asilimia 86 ambayo ni theluthi moja zaidi ya siagi.

Hata hivyo, si mara ya kwanza mafuta ya nazi kutajwa kuwa hatari katika afya ya binadamu, baada ya mwaka 2005  ikiwa ni miaka 13 iliyopita, Shirika la Afya Duniani (WHO), liliorodhesha mafuta  hayo kuwa miongoni mwa vyakula ambavyo havifai kutumiwa kama chakula kama hutaki kupatwa na matatizo ya shinikizo la moyo.

Pia miaka ya 90 kulikuwa na tahadhari ya kiafya nchini Marekani, wakati utafiti ulipodai kwamba mahindi ya kukaanga maarufu kama ‘popcorn’ zinazotumika wakati watu wanapotazama filamu zina mafuta kwa sababu zilikuwa zikipikwa kwa kutumia mafuta ya nazi.

Kwa mujibu wa tafiti kutoka taasisi za Marekani zinazojishughulisha na matatizo ya moyo zilizotolewa mwaka jana, takribani asilimia 72 ya raia wa Marekani wanaamini kwamba, mafuta ya nazi yana afya, japokuwa katika kiwango hicho ni asilimia 37 ya wataalamu wa lishe bora wanaokubali.

Walieleza kuwa inatokana na kampeni nzuri kutoka kwa kampuni za kuuza mafuta hayo ambazo zinasema kuwa yanaweza kutumika kama mbadala wa siagi na mafuta yanayotokana na mimea mbali na ithibati kutoka kwa watu maarufu kama Gwyneth ambaye amepiga debe kutumia kama chakula bali pia kutumia kama mafuta ya kupaka uso na nywele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles