27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

MAFUTA YA KUPIKIA YAPANDA BEI

TUNU NASOR NA JULIETH JULIUS-DAR ES SALAAM


BEI ya mafuta ya kupikia imepanda kutoka Sh 2,500 kwa lita hadi Sh 3,500 MTANZANIA limebaini.

Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA jana katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam umebaini kuwa lita moja ya mafuta ya kula imeongezeka, huku ndoo ya lita 20 ikiuzwa kati ya Sh 55,000 na 60,000 badala ya Sh 52,000.

Katika maeneo ya Tandale na maduka yaliyopo katika mitaa ya Sinza na Manzese, ongezeko hilo limeongeza ukali wa maisha kwa watu wengi hasa wa hali ya chini kutokana na kuendelea kupanda kwa bei ya vyakula inayochagizwa na ukame katika mikoa mbalimbali nchini.

Soko la jumla la Tandale, mchele unauzwa kwa bei ya jumla kati ya Sh 200,000 na 220,000 kwa gunia moja lenye kilo 100, huku kilo moja ikiuzwa kati ya Sh 2,400 na 2,500.

Mahindi yamepanda kutoka wastani wa Sh.120,000 hadi 180,000 kwa gunia moja la kilo 100, huku kilo moja ya mahindi ikiuzwa kwa Sh. 2,000.

Mfuko wa unga wa mahindi wenye kilo 25 ambao awali ulikuwa ukiuzwa kwa Sh 22,000 na baadaye uliuzwa  kwa Sh 35,000 hivi sasa unauzwa Sh 40,000 na kilo moja ikiuzwa kwa Sh 2000 badala ya Sh 1500.

Maharage gunia moja linauzwa Sh 200,000 hadi 250,000 kulingana na ubora wake, wakati kilo moja inauzwa Sh 2,600 hadi Sh 3,200.

Akizungumzia kupanda kwa bei hizo, mmoja wa wateja wa  bidhaa hizo, Neema Mmbaga alisema familia yake imebadili mfumo wa kula ambapo hivi sasa wanakula mara moja kwa siku.

“Inatubidi kula mara moja kwa siku kutokana na upatikanaji wa fedha kuwa mgumu na vyakula kuendelea kupanda kila kukicha,” alisema Neema. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles