29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

MAENEO MATATU KIKWAZO HOTUBA YA LEMA BUNGENI

Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema, akisoma Hotuba ya Bajeti mbadala ya wizara hiyo ya Mwaka 2017/2018 bungeni Dodoma jana. Picha na Deus Mhagaale.

 

 

Na MAREGESI PAUL-DODOMA

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, ameendelea na utaratibu wa kuhariri hotuba za Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni baada ya kufanya hivyo katika hotuba iliyosomwa jana na Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema.

Kutokana na hali hiyo, Lema alizuiwa kusoma maeneo matatu katika hotuba yake yaliyodaiwa kukiuka kanuni za Bunge. Maeneo hayo yalihusu rushwa, utesaji wa watu pamoja na watu kupotezwa.

Kuzuiwa kwa hotuba hiyo ni mwendelezo wa baadhi ya hotuba za upinzani bungeni kuzuiwa kwa kile kinachodaiwa kuwa wanakiuka kanuni za kudumu za Bunge.

Hotuba ya kwanza kuzuiwa ilisomwa mwezi uliopita na Mbunge wa  Malindi, Ally Saleh (CUF) iliyohusu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na kufuatiwa na hotuba ya Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu.

Wiki iliyopita, hotuba ya Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi (maarufu kwa jina la Sugu) nayo ilizuiwa na kuzua mvutano kati ya Sugu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu.

Kutokana na hali hiyo, wiki iliyopita Spika Ndugai alikemea tabia hiyo na kuwalalamikia waandishi wa hotuba za upinzani ambao wanalipwa na Bunge, waache uandishi huo kwa sababu haiwezekani awalipe mshahara na baadaye waandike hotuba za kuushutumu muhimili huo.

Katika tukio la jana, awali Mwenyekiti wa Bunge, Najma Murtaza Giga, aliliambia Bunge kwamba amepewa maelekezo na Spika, akimtaka Lema asisome baadhi ya maeneo yaliyodaiwa kukiuka kanuni za Bunge yaliyomo katika hotuba yake.

Hata hivyo, katika maeneo aliyosoma, Lema alilalamikia ofisi na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kwamba inasababisha msongamano na mateso magerezani kutokana na jinsi inavyofanya kazi kwa kutofuata sheria.

“Chanzo muhimu kinachosababisha msongamano na mateso magerezani ni ofisi ya DPP, sheria mbovu, zisizozingatia utu na ucheleweshaji wa upelelezi kutoka Jeshi la Polisi.

“Ofisi ya DPP tangu Serikali ya awamu ya nne iingie madarakani, imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali zenye nia ovu za kuitumia mahakama ndivyo sivyo kwa kupindisha haki kwa makusudi katika kesi mbalimbali.

“Ofisi hiyo imekuwa ikizuia haki ya dhamana kwa watuhumiwa ambao hawajatiwa hatiani na mahakama kwani hudiriki kufanya hivyo hata katika makosa ambayo kisheria watuhumiwa wana haki ya kupata dhamana,” alisema Lema.

Kuhusu kitengo cha usalama barabani cha Jeshi la Polisi, Lema alikilalamikia na kusema askari wake wanafanya kazi kwa mazoea kwa kuwa hawajapata mafunzo ya kazi zao kwa muda mrefu.

Kutokana na hali hiyo, alisema kuna haja sasa masuala yanayohusu usalama barabarani, yakaanza kufundishwa kuanzia shule za msingi hadi katika vyuo vya elimu ya juu kutokana na umuhimu wake.

“Tuna taarifa kwamba, mafunzo ya askari wa usalama barabarani, hayajafanyika kwa muda mrefu kutokana na ukosefu wa fedha na hivyo kuwafanya askari hao kufanya kazi kwa kuvizia magari ikiwa ni pamoja na kupanda mwenye miti wakiwa na kamera za tochi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles