26 C
Dar es Salaam
Monday, January 17, 2022

Maelfu ya wanawake, wasichana wauzwa Mali


Nigeria

Inahofiwa wanawake na wasichana 20,000 wameuzwa kutoka Nigeria, kwenda Mali na kulazimishwa kufanya biashara ya ukahaba.

Mkuu wa Kupambana na Biashara ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu wa Nigeria, Julie Okah-Donli, amesema mamia ya wanawake na wasichana wengi walirejea kutoka eneo la kusini mwa Mali la Kangaba miezi michache iliyopita.

Timu iliyotumwa kufanya uchunguzi eneo hilo ilibaini wasichana wengi kutoka nchini Nigeria wamekuwa wakishikiliwa maeneo hayo.

Wasichana hao walio na umri wa kati ya miaka 16 na 30 hupewa ahadi za kutafutiwa kazi katika nchi ya Malaysia, lakini hujikuta wakiingizwa katika biashara ya ukahaba.

Okah-Donli, anasema wengi wanashikiliwa katika mazingira hatarishi na ya kitumwa na hawawezi kutoroka kwa sababu wamewekwa maeneo ya mbali.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,717FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles