30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Maelfu washikiliwa kwa kuandamanaUfaransa

PARIS, Ufaransa

WATU  wapatao 1,726 walikamatwa na  polisi  kufuatia maandamano yaliyoikumba nchi hii  wiki iliyopita katika maeneo mbalimbali kupinga ongezeko  la kodi katika bidhaa mbalimbali hususan za mafuta.

Taarifa  hiyo metolewa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Christophe Castaner  na akasema waandamanaji  1,220  waliwekwa rumande na wengine 619 wamshafunguliwa mashtaka.

Waziri huyo alisema waandamanaji wengi walikutwa na silaha ingwa mawakili wao wanadai kuwa hawakuwa na vitu kama bali waliandamana kuonesha hisia zaoa kali na wala hawakufanya vurugu zozote.

Waziri huyo alisema kuwa wengi wa waandamanaji ambao wanawashikilia mahabusu wanatuhumiwa kufanya vurugu ama kuhamasisha uharifu.

Jumamosi hiyo ilishuhudiwa maandamano mengine ya nne yanayowahusisha watu wanaohitwa vizibao vya njano ambao wanapinga kuongezwa kwa bei ya mafuta, kodi na ghrama za maisha.

Katika jiji hili la Paris, Lille, Lyon, Marseille, Nantes  na  Toulouse waandamanaji hao walipambana na polisi na kati yao  135 walijruhiwa mjini hapa.

Maandamano hayo yalianza baada ya Novemba 17 mwaka huu serikali kutangaza kuwa bei yha mafuta ya petroli  na dizeli nchini itapanda kuanzia  Januari mosi  mwakani senti Euro 3  kwa petrol na senti Euro  6.5 kwa dizeli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,391FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles