23 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

Maelfu wamiminika kwenye maandamano

GAZA, PALESTINA

WIMBI kubwa la waandamanaji wa Kipalestina, jana walianza rasmi maandamano makubwa katika Ukanda wa Gaza mashariki karibu na mpaka na Israel kuadhimisha mwaka mmoja tangu yalipofanyika maandamano makubwa ya aina yake ya kudai haki ya kurudi kwa wakimbizi wa Kipalestina. 

Mamia kwa maelfu wanatarajiwa kujiunga na maandamano hayo katika kipindi cha siku nzima leo. Tangu asubuhi na siku kadhaa zilizopita kundi la Hamas limekuwa likitoa mwito kwa kutumia vipaza sauti kuwataka watu wa Gaza kujitokeza kushiriki katika maandamano hayo. 

Duru za hospitali za Gaza zimesema Mpalestina mmoja aliyekuwa miongoni mwa waandamanaji alijeruhiwa katika mapigano yaliyotokea kati yao na wanajeshi wa Israel Mashariki mwa mji wa Gaza na baadaye kufariki jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,800FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles