24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MADUU WANAOPETA BILA KIKI, SKENDO BONGO FLEVA

Na CHRITOPHER MSEKENA

“@officialshetta ndugu yangu, najua unanionea gere mwenzako toka juzi Insta yote imehamia Madale… na wewe unataka kuingia kwenye huu upepo wa #Muzikisiasa… we usijiulize ingia tu, maana mjini sasa hivi vingoma vya mapenzi vigumu, ikiwezekana jifanye unataka kumtolea mahari Mange umuoe…kesho mji wote wako ila kuna mawili, sentro au matusi.”

Hayo ni maneno ya utani aliyotoa wiki hii staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ akimtania msanii mwenzake Nurdin Bilal ‘Shetta’ ikiwa ni siku moja tu tangu aachie ngoma yake ‘Acha Nikae Kimya’, wimbo uliozua gumzo nchini.

Kwa utani huo unaweza kuona ni namna gani matukio (kiki) yanavyooanishwa na kazi za sanaa ambapo mastaa kadha wa kadha wamekuwa na utamaduni wa kutengeneza matukio bandia kabla hawajatoa kazi mpya ili kuwasogeza karibu mashabiki.

Ni mtindo unaotumiwa na mastaa wengi ulimwenguni kote, siyo jambo geni kabisa.

Ingawa si wasanii wote hutumia kiki kuongeza usikivu kwa mashabiki, kwa upande wa wasanii wa Bongo Fleva kuna  sampo hiyo ya wasanii wasioendeshwa kwa kutumia kiki.

Hapa chini nakupa listi ya wasanii wa kike wa Bongo Fleva ambao kiki kwao siyo dili, wanapiga kazi tu. Mastaa hawa  hawatoi nafasi ya kiki kuendesha muziki wao.

Swaggaz tunawapa heshima warembo hao na hapa tunakusogezea baadhi tu ya mastaa wapya wa kike ambao hawatumii kiki kwenye kazi zao za sanaa bali kazi zao nzuri ndiyo zinazowakiki mbele ya jamii.

 

MAUA SAMA

Huyu ni mwimbaji hodari ya nyimbo za mapenzi, ana sauti nyororo anayoitumia vyema kuumudu ushindani uliopo kwenye Bongo Fleva. Anamiliki hit song kali kama ‘So Crazy’, ‘Let Them Know’, ‘Sisikii’, ‘This Love’, ‘Mahaba Niue’ na ‘Main Chick’.

Zaidi ya muziki wake kumpa kiki kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva mpaka kuchukua tuzo ya Wimbo Bora wa Reggae (Let Them Know), hajawahi kufikiria kutengeneza tukio ili kubusti kazi zake.

 

NANDY

Mrembo huyu ni balozi wa taasisi iliyoanzishwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson. Heshima ambayo imekuja baada ya kuonekana msafi ambaye hana makandokando kwenye maisha ya ustaa.

Ubalozi ni dili ambalo wasanii wengi wa kike wamelikosa kutokana na skendo au kiki ambazo mwisho wa siku zimeondoa heshima yao. Nandy amekuwa staa kutokana na mashabiki kumpa usikivu kupitia nyimbo zake kama ‘Nagusagusa’ na ‘One Day’.

 

ROSA REE

Kutoka The Industry, lebo inayomilikiwa na Kundi la Navy Kenzo tunakutana na rapa mwenye sauti na michano yenye mamlaka, Rosa Ree ambaye hivi karibuni aliungana na Rick Ross katika dili la ubalozi wa kinywaji cha Luc Beraile.

Kiki siyo sehemu ya maisha yake sababu uwezo wake wa kuchana pekee ni kiki tosha kwenye muziki wa Hip Hop kiasi kwamba rapa mkubwa kama Joh Makini amemtabiria makubwa huko mbeleni.

 

MIMI MARS

Anaitwa Marianne Mdee ambaye ni mdogo wa damu wa Vanessa Mdee. Ni mtangazaji ambaye amejiongeza kwa kutumia talanta yake ya pili ya uimbaji na sasa anasumbua na ngoma inayoitwa Shuga.

Hapendi sana kutumia mgongo wa dada yake ili kufika kwenye kilele cha mafanikio. Anatambua kiki siyo afya kwa uhai wa muziki wake ndiyo maana amekaza kwa kufanya kazi nzuri zilizompa mashabiki wa kutosha.

CHEMICAL

Ni nadra msichana mdogo kujiamini kiasi kile, rapa Chemical ni alama ya warembo wote wenye ujasiri wa kukabili hali zote zilizopo kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Ni muwazi na mkweli, asiyependa kupindisha mambo. Hajawahi kutumia kiki ili kusukuma ngoma zake. Skendo pia huwa anazikwepa kwa sababu hataki kuzichanganya na muziki alioujenga kwa miaka mitatu sasa.

Mfano ni kipindi kile msanii Stereo alipotangaza hadharani kumpenda, Chemical aliutatua msala ule bila kuacha madhara kwenye muziki wake.

Chukueni tano wote!

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles