24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 30, 2023

Contact us: [email protected]

Madrid kunusurika kifungo Copa del Rey

25586MADRID, HISPANIA

RAIS wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez, amesema timu yake ipo salama na itaendelea kushiriki michuano ya Copa del Rey, japokuwa ilimtumia mchezaji ambaye alitakiwa kutumikia kadi za njano ambazo alipewa mwishoni mwa msimu uliopita.

Katika mchezo wa katikati ya wiki hii, Madrid walimtumia mchezaji wao, Denis Cheryshev, ambaye alikuwa na kadi tatu za njano katika mchezo wa mwisho msimu uliopita, hivyo alitakiwa asicheze katika mchezo wa Jumatano wiki hii, lakini Madrid walimchezesha na kupachika bao la kwanza dhidi ya Cadiz.

Hata hivyo, rais huyo amesema kuwa hawakupewa taarifa yoyote ya kutomtumia mchezaji huyo, hivyo wanaamini watakuwa salama.

“Tulikuwa hatuna taarifa yoyote kwamba mchezaji huyo anatakiwa kukosa baadhi ya michezo kutokana na kadi ambazo alizipata wakati yupo Villarreal kwa mkopo, bado hatukupewa taarifa yoyote kutoka kwa Shirikisho la Soka nchini Hispania (RFEF).

“Bado tupo salama na tutaendelea kushiriki michezo yote ya Copa del Rey kwa kuwa iko wazi hatukuwa na taarifa yoyote,” alisema Perez.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,285FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles