29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani waagiza mhandisi wa maji afukuzwe

Rajabu MtiulaNa AMON MTEGA, SONGEA

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Songea, limeagiza Kaimu Mhandisi wa Maji wa halmasahauri hiyo, John Undili, afukuzwe kazi.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Rajabu Mtiula, alipokuwa akizungumza katika kikao cha baraza hilo mwishoni mwa wiki.

Katika taarifa hiyo, Mtiula alisema wamelazimika kuchukua hatua hiyo kwani Undili anadaiwa kutumia vibaya fedha za miradi ya maji.

Alisema mtumishi huyo wa umma, kwa nyakati tofauti alifanya ubadhirifu na kuisababishia halmashauri hasara ya Sh milioni 41.6 na kusababisha miradi ya maji iliyokuwa itekelezwe katika vijiji vya Parangu, Matimila, Mpitimbi na Magagura, isitekelezwe.

“Pamoja na kwamba tumechukua hatua hiyo, bado tutaendelea kuchukua hatua dhidi ya watumishi watakaothibitika kutumia vibaya fedha za umma.

“Kwa hiyo baada ya sisi kuchukua uamuzi huu, tunaamini utatekelezwa na mhusika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili,” alisema Mtiula.

Mwenyekiti huyo wa halmashauri aliwataka pia watumishi na watendaji katika halmashauri hiyo, wahakikishe wanafanya kazi kwa uadilifu na umakini ili wasichukuliwe hatua.

Wakati huo huo, Mtiula alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Simon Bulenganija, ahakikishe ofisi za halmashauri hiyo zinahamia eneo la Lundusi kama alivyoagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene.

Kwa mujibu wa Mtiula, mtumishi yeyote atakayekwamisha uhamisho hao, atachukuliwa hatua kwa kuwa hakuna muda wa kubembelezana serikalini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles