28.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 2, 2021

Madiwani Lindi waaswa kuacha itikadi zao

Hadija Omary, Lindi

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani hapa, wametakiwa kuacha itikadi za vyama vyao badala yake wadumishe mshikamano kwa maslahi ya manispaa yao.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Lindi, Saidi Madebe alipokuwa akitoa salamu za chama hicho juzi katika kikao cha robo ya pili cha Baraza la Madiwani.

Madebe amesema ili manispaa hiyo iwe na maendeleo ni vyema madiwani wakawa na ushirikiano wenyewe kwa wenyewe pamoja na watumishi wengine.

“Sisi ndiyo tuliopewa dhamana na wananchi hivyo ni vizuri tukiwa tunashirikiana pamoja na kushirikishana katika shughuli za kuwaletea maendeleo wananchi wetu  ikiwa pamoja na kubuni kwa pamoja mbinu mbalimbali za kuongeza kipato ndani ya halmashauri yetu,” amesema Madebe.

Madebe amesema kwa kuzingatia kuwa manispaa yao kuwa masikini wa vyanzo vya mapato ni vyema madiwani na watumishi kubuni mbinu mbali mbali za kuanzisha miradi ya uvunaji wa mazao ya bahari au mashamba.

“Kutokana na uhalisia wa halmashauri yetu njia kubwa ya kuongeza kipato ni hiyo kupitia bahari na mashamba hivyo ni vyema ni kubuni miradi au kutafuta wawekezaji ili kuwekeza katika eneo hilo kwa hakika mkishirikiana kwa pamoja kwa wazo ili au jingine tunaweza kuongeza kuongeza vyanzo vya mapato pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi wetu,” amesisitiza Madebe.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,663FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles