28.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 30, 2023

Contact us: [email protected]

Madiwani Jiji la Dar waomba mafunzo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wameomba wapatiwe semina mbalimbali za kuwajengea uwezo katika utekekezaji wa majukumu yao.

Hayo yalisemwa wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo wakati wa kupokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2019/2020.

Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika kikao cha baraza wakati wa kupokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akizungumza katika kikao hicho, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, amesema siri ya iliyokuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kupata hati safi mfululizo kwa kipindi cha miaka mitano imechangiwa na semina mbalimbali na mafunzo ya kuwajengea uwezo madiwani hasa katika kusimamia miradi ya maendeleo na wamekuwa wakifanya vizuri katika usimamiaji wao.

“Naomba madiwangu wangu wote wapate mafunzo ili waweze kuleta maendeleo ya kutosha watekeleze majukumu yao vizuri katika usimamiaji miradi mbalimbali ambayo inapitishwa na halmashauri yao,” amesema Kumbilamoto.

Akizungumza hati safi Meya Kumbilamoto amesema kwa kuwa wamepewa hadhi ya jji na Serikali watashirikiana vizuri na madiwani na watendaji katika kusimamia mapato na miradi ya maendeleo.

Amesema kabla ya kuvunjwa kwa iliyokuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilipata hati yenye mashaka. Jiji hilo lilivunjwa Februari 24,2021 na taarifa ya CAG ilitoka Machi 31,2021.

Baraza hilo la madiwani limepitia taarifa hiyo na kuelekeza kuwa hoja ambazo hazijafungwa zifanyiwe kazi na kuwasilishwa kwa CAG kwa ajili ya uhakiki huku likisisitiza pia kufanyika uhakiki wa kina kwa hoja ambazo hazijafungwa kwani zinahusu mali ambazo zimegawanywa katika halmashauri mbalimbali.

Baraza hilo lilielezwa kuwa hoja zilizowasilishwa ni 26, zilizofungwa 6 sawa na asilimia 23 na zinazoendelea kufanyiwa kazi ni 20 sawa na asilimia 77.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,198FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles