24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani Iringa sasa ni mwendo wa kidigital

Na Rayomnd Minja, Iringa

Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoani Iringa imegawa vishikwambi (tablets)16 kwa madiwani wake ili viweze kuwarahisishia kupata makabrasha ya vikao na kuyapitia kabla ya kukutana kwenye Baraza.

Akizungumza wakati ugawaji wa vishikwambia hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Happiness Laizer amesema walimaua kununua vifaa hivyo ili kuwarahisishia kazi madiwani ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za uandaaji wa makabrasha hayo.

Laizer amesema ema kuwa vifaa hivyo kila kimoja kimenunuliwa kwa Sh 870,000 hivyo vishikwambi hivyo vyote kwa ujumla vimegharimu Sh milioni 14.

“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya tuliamua kufikia maamuzi haya ya kununua hivi vifaa kwani awali tulikuwa tunaanda makabrasha kwa kuyachapisha na kuanza kutembeza, kuyasambaza kwa madiwani lakini sasa kwa kutumia vifaa hivi tutarahisisha hiyo kazi.

“Tutakuwa tunawatumia waheshimiwa madiwani makabrasha kwenye vifaa hivyo na kuyapitia kwa wakati na kwa urahisi zaidi,” amsem Laizer.

Amesema kwa kutumia vifaa hivyo itasaidia kupunguza gharama za uchapishaji waliokuwa wakitumia hapo awali lakini pia kuanza kuyasambaza kwenye kila kata ya diwani husika kwa kutumia magari ya halmashauri.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Saadi Mtambule aliipongeza halmashauri hiyo kwa kuamua kwenda kidigital kwani itawarahisishia kufikisha taarifa kwa wakati kwa madiwani.

Amesema dunia ya sasa imegeuka kuwa kijiji na kwenda kisasa hivyo vifaa hivyo ni muhimu sana kwa mustakabali wa maendeleo ya halmashauri hiyo.

“Sasa hivi ni ulimwengu wa kidigitali na ndio maana tuliona hata kipindi cha Uviko 19 hakukuwa na vikao kama hivi watu walikuwa wanatumia tekinolojia, hivyo hata nanyi naamini sasa mtafanya shughuli zenu vizuri bila ya kuwa na vikwazo vyovyote kwani hata hakutakuwa na malalamiko ya kucheleweshewa makabrasha ya vikao,” amesema Mtambule.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Reginali Kivinge amesema vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka kwani awali madiwani wengi walikuwa wanalalamika kutokupata makabrasha kwa wakatii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles