27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani Iramba wapitisha rasmu ya bajeti Sh bilioni 41.16

Na Seif Takaza, Iramba

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida limepitisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2022/2023.

Mpango huo umepitishwa katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika jana  katika ukumbi mdogo wa Halmashauri hiyo ambapo limepitisha Rasimu ya Bajeti yenye makisio yenye thamani ya Sh bilioni 41.16 katika bajeti hiyo kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato.

 Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Michael Matomora amesema katika rasimu fedha kutoka mapato ya ndani Sh bilioni 5.38 ruzuku ya Serikali ni Sh bilioni 25.4 huku wahisani ikiwa ni Sh bilioni 10.3.

Amesema mwaka ujao wa fedha wa 2022/ 2023 halmashauri hiyo imekisia kutumia jumla ya Sh bilioni 41.16 kutokana na vyanzo mbalimbali.

Amesema kutoka mapato ya ndani wametenga Sh milioni 23.52 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, Sh bilioni 2.143 miradi ya maendeleo Sh bilioni 3.21 huku jumla  ya mapato ya ndani ikiwa ni Sh bilioni 5.38..

Akielezea ruzuku ya serikali amesema mishahara ni Sh bilioni 20.4, matumizi ya kawaida Sh. bilioni 1, miradi ya maendeleo Sh bilioni 3.9 jumla ikiwa ni Sh bilioni 25.40.

Alitaja fedha kutoka kwa wahisani kuwa ni Sh bilioni 10.37 huku jumla yake ikiwa ni Sh bilioni 41.16.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iramba, Innocent Msengi aliwapongeza madiwani kwa kupitisha rasimu hiyo ambayo ameitaja kuwa ni ya kipekee na ya mfano.

“Nitumie nafasi hii kuwapongeza madiwani kwa kuandaa rasimu hii nzuri na ya kipekee hivyo nawaombeni mkaitekeleze katika kukusanya mapato ili tuwenze kusonga mbele,” alisema Msengi.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda alishukuru madiwani hao kwa kupitisha rasimu hiyo na akatumia nafasi hiyo kuwaomba madiwani hao kwenda kuhimiza wananchi wao kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la sensa ya watu na makazi na anuani za makazi.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Iramba, Ephrahimu Kolimba aliwaomba madiwani hao kwenda kuzisimamia vizuri fedha hizo na akataka kuwepo na mashindano ya kuwashindanisha kwa utendaji kazi wao na washindi wapatiwe zaidi pamoja na wananchi wao waliofanya kazi husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles