25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 6, 2022

Contact us: [email protected]

Madiwani Ilala waikataa bajeti 2016/17

Charles KuyekoNA CHRISTINA GAULUHANGA,DAR ES SALAAM

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jana liliingia dosari baada ya wajumbe wa kamati mbalimbali kugomea mapendekezo ya bajeti ya manispaa hiyo kwa mwaka 2016/ 2017 wakidai yamechakachuliwa.

Wajumbe hao kwa nyakati tofauti walisimama na kumtaka Mwenyekiti wa Baraza hilo, Meya Charles Kuyeko kuhakikisha anaahirisha baraza hilo ili Mchumi na Mkurugenzi, Isaya Mngurumi wakayapitie mapendekezo ya wajumbe hao na kuyaingiza kwenye nyaraka zilizowasilishwa kwa wajumbe hao kwa ajili ya majadiliano.

“Mimi mjumbe wa kamati ya Ukimwi mambo mengi tuliyoyajadili na kuyapendekeza humu hayamo na
hatukubali kuendelea na baraza hilo,” alisema Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema).

Alisema kikao cha jana kilikuwa na kasoro nyingi ikiwamo ucheleweshaji wa nyaraka ambazo wajumbe walipewa wakiwa ndani ya kikao na hivyo kutopata muda wa kuzipitia.

Baadhi ya upungufu uliojitokeza katika bajeti hiyo ni katika kamati za fedha, mipango miji na mazingira na Ukimwi.

Wajumbe wa baraza hilo kwa nyakati tofauti walisema inabidi mkurugenzi abadilike na kwamba kama baraza lililopita lilikuwa la ndiyo hili ni la aina nyingine.

Mkurugenzi Mngurumi alisema kama wajumbe wanagomea mapendekezo hayo, pia wawe tayari kurejesha posho za vikao vya kamati.

Hadi tunakwenda mtamboni jana usiku, madiwani hao walikuwa wamegoma kuijadili bajeti hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,603FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles